Posts

SHUHUDIA DK. MAGUFULI ALIVYORUDISHA FOMU ZA URAIS NEC LEO

Image
  Mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damiani Lubuva, wakati alipowasili ofisi hizo. …Akiwa na mgombea mwenza, Samiah Hassan Suluhu. Viongozi wa CCM waliomsindikiza mgombea wao wa urais. Lubuva (kulia) akizungumza jambo wakati wa kurudisha fomu hizo. Magufuli akionyesha fomu wakati wa kurudisha. Mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya kurudisha fomu. Wanahabari wakiwa kazini katika hafla hiyo. Magufuli akitoka ofisi za NEC baada ya kukamilisha zoezi hilo. MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli, leo amerudisha fomu ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). NEC iliwataka wagombea wote wa urais kupitia vyama vyote vya siasa kurudisha fomu leo Agosti 21 baada ya kuzunguka mikoa ya Tanzania kutafuta wadhamini, ambapo vyama vyote hivyo viwili vimeonekana kukidhi vigezo na kurudisha fomu hizo. (PICHA: DENIS MTIMA/GP

LOWASSA, DUNI WARUDISHA FOMU TUME YA UCHAGUZI LEO, SASA NI WAGOMBEA RASMI

Image
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza mara baada ya kupokea Fomu zilizorudishwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni baada ya kukamilisha mchakato wa kutafuta wadhamini katika Mikoa 10 ya Tanzania na kutimiza masharti yote ya Uchaguzi, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akimkabidhi, Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, nyaraka mbalimbali zitakazotumika wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam leo Agosti 21, 2015. Kushoto ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.CHANZO OTHMANI MICHUZI Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowas

MAGUFULI ASAINI HATI YA KIAPO YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU JIJINI DAR

Image
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli  akikabidhi hati ya Kiapo mapema leo mchana kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Sekieti Kihiyo (katikati). Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.  Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli akisaini hati ya Kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.  Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Jaji Sekieti Kihiyo mara baada ya  kusaini hati ya kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Sami

KIPINDUPINDU CHAENDELEA KUTESA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
 Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Nusura Kessy (kushoto), akiwaelekeza wauguzi wa saidizi wake namna ya kuchanganya dawa maalumu ya kuondoa vijiji vinavyoweza kuwa vya ugonjwa wa kipindupindu katika kambi ya wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi. Katika kambi hiyo kuna wagonjwa 21 kati yao watoto ni 7.  Vyombo vikiwekwa kwenye dawa.  Muuguzi Msaidi wa Zahanati ya Mburahati, Maimuna Pazi (kushoto) na Mlinzi wa Zahanati hiyo, Abdallah Mbagala wakisaidiana kuweka dawa maalumu ya kuzuia kuenea kwa vijidudu vya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu katika vyombo walivyoletewa chakula na ndugu zao katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo katika Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi. Dawa hiyo maalumu ikiwekwa katika vyombo vya kutumia. Na Dotto Mwaibale HALI ya ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba maeneo kadhaa ya jiji bado inaonesha ni tete kufuatia ida

Jokate: Wazazi wasiingilie mapenzi ya watoto

Image
Staa wa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’. Brighton Masalu SIKU chache baada ya gazeti dada ya hili la Ijumaa Wikienda kuripoti juu ya wazazi wa Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ kumkataa Ali Kiba kama mchumba wake, binti huyo ameibuka na kuwataka wazazi kote nchini kuacha kuwaingilia watoto wao katika masuala ya kimapenzi, akidai jambo hilo ni vema wakiachiwa wenyewe. Akizungumza na gazeti hili, Jokate alisema ni vyema kama wazazi wakawaacha watoto wao waoe au kuolewa na watu wawapendao, kwani vinginevyo ni kuwaingilia maisha na uhuru wao binafsi, jambo ambalo si jema. “Unajua nimelala, madai ya Ally (Kiba), sitaki kuyazungumza sana, unajua mimi ni binti mtu mzima, ninao uhuru wa kumchagua nimpendaye kwa ajili ya maisha yangu, ifike mahali wazazi wawape uhuru watoto wa kufanya mambo yao, awamu hii siko tayari kuona naumizwa tena na familia juu ya uhusiano wangu,” alisema binti huyo kwa njia ya simu juzi.

Lulu amchokonoa Zari

Image
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’  akiendelea ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Mwandishi Wetu UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya bethdei ya DJ wa Diamond, Rommy Jones. Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo. Mastaa mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo. ILIANZA HIVI Lulu, alikuwa wa

HIKI NDICHO ALICHOKIJIBU ZARI THE BOSS WA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU MPANGO WA IVAN NA KING LAWRENCE

Image
Hatimaye Zari The Bosslady ameamua kumjibu ex wake Ivan na swahiba wake King Lawrenc ambao wamekuwa wakimtupia madongo kuwa mtoto wake Tiffah si wa Diamond, ni wao. King Lawrence alienda mbali zaidi kwa kutumia kampuni ya wanasheria kumtaka achukue vipimo vya DNA vya kichanga hicho chenye zaidi ya followers 80k kwenye Instagram. Zari ametumia Instagram kuwajibu kwa kudai kuwa wanachofanya wawili hao ni visasi ambavyo anaamini hufanywa na vilaza! “Visasi hufanywa na vilaza,” ameandika Zari kwenye Instagram. “BO$LADY anafahamu kuwa huzuni aliyonayo mtu mwenye chuki wakati akiangalia furaha na mafanikio yake ni adhabu tosha. Inabidi niyageuzie mgongo mambo yate ya kijinga yanayoendelea. Naendelea kuwaua kwasababu watu hutaka kuzima taa inayowaka zaidi kwao,” ameongeza. Diamond tayari ametoa majibu yake kufuatia hatua hiyo ya Ivan na Lawrenc

Asasambua mchana kweupe kumkomesha mchepuko

Image
M UME wa mtu sumu! Kitendo cha wanawake kutembea na waume za watu ni cha kawaida kabisa katika maeneo mengi nchini na wengi wamejikuta wakikutana na balaa, lakini tabia hiyo inaendelea kila kukicha. Samora Abdallah (pichani), Afisa Mtendaji wa Mtongani, Kata ya Mbuyuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam, anao mkasa wa kusisimua ambao ni moja kati ya kesi nyingi alizopata kuzifanyia kazi ofisini kwake kama anavyosimulia; “Hata sijui nianzie wapi, kuna siku kundi la watu walifika ofisini kwangu, nilipohoji ujio huo kwa kuwa haukuwa wa amani, nikajibiwa kwa kuoneshwa kidole kwa dada mmoja aliyeshukiwa kuchukua mume wa mwenzie. Mara wakaanza kurushiana maneno machafu, nusura wakunjane, nikawazuia na kutaka kujua kulikoni. “Dada mmoja akaniambia kuwa binti aliyekuwa mbele yetu, anatembea na mumewe kwamba siku hiyo aliichukua namba yake kutoka kwenye simu ya mume wake na kuanza kuchat naye akijifanya ndiye yeye. Alizungumza naye mambo mengi na mwishowe akamtaka aje sehemu

HARUSI YA MENINA ILIYOFUNGWA KWA SIRI KUBWA NIMEKULETEA PICHAZ HAPA TOKA AKIPAMBWA SALOON HADI KITU CHA MKEKANI!! UNAMJUA MUMEWE LAKINI ALIYEBEBA JIKOOOO

Image

CCM YATANGAZA RASMI KIKOSI CHAKE CHA KAMPENI 2015 JIJINI DAR LEO

Image
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa kamati ya Kampeni  kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015,ambayo itaongozwa   na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Wajumbe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto. Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja  na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto). Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi

MANCHESTER UNITED WAITANDIKA CLUB BRUGES GOLI 3 KWA 1

Image

BREAKING NEWS: PROF. KITILO AKATAA KUGOMBEA URAISI ACT, BARUA YAKE HII HAPA

Image
Ndugu Wazalendo, Naomba niwashukuru nyote kwa imani kubwa mliyo nayo juu yangu katika kukiwakilisha chama katika nafasi ya Rais. Naishukuru pia Kamati Kuu kwa imani yake kwangu hata kufikia hatua ya kupitisha azimio la kuniomba nigombee urais kwa chama chetu. Jana Kamati Kuu ilituma ujumbe maalumu nyumbani kwangu kwa ajili ya kuzungumza na familia na jamaa zangu juu ya ombi hili. Aidha, Nimekuwa nikilitafakari jambo hili tangu Alhamisi nilipoombwa rasmi kutafakari uwezekano wa mimi kugombea baada ya juhudi zetu za kutafuta mgombea kushindikana. Nimefanya mawasiliano mapana katika familia, ndani ya chama, chuoni ninapofanyia kazi, Kanisani kwangu,na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo. Baada ya tafakari na mawasiliano  CONSULTATIONS  mapana nasikitika kusema kwamba sina utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia, na kisiasa kuniwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huu. Najua nimewaangusha sana katika uamuzi wangu huu

HIVI NDIVYO MABASI YA MWENDO KASI YALIVYO ZINDULIWA JIJINI DAR

Image
Moja ya mabasi yaendayo mwendo wa haraka yakiwa barabarani katikati ya jijini Dar es Salaam leo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi wa semina ya mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es salaam, juu ya kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi huo Oktoba mwaka huu, Semina itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) waliokaa mbele, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki na kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi. Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia aliyeshika mkasi akikata utepe kuzindua mafunzo madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mafunzo yayo ya madereva. Baadhi ya viongozi wa jesh