HIVI NDIVYO MABASI YA MWENDO KASI YALIVYO ZINDULIWA JIJINI DAR

Moja ya mabasi yaendayo mwendo wa haraka yakiwa barabarani katikati ya jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi wa semina ya mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es salaam, juu ya kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi huo Oktoba mwaka huu, Semina itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) waliokaa mbele, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki na kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi.
Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia aliyeshika mkasi akikata utepe kuzindua mafunzo madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mafunzo yayo ya madereva.
Baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi hapa nchini wakiwa na abiria katika basi la mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi na Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi katika mradi wa mafunzo ya madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka (BRT) jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii. 
Na Mwandishi wetu.
SERIKALI imewataka madereva walioanza kupata mafunzo ya kuendesha mabasi yatakayotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) kuzingatia mafunzo hayo ya kihistoria hapa nchini.
Mafunzo hayo yaliyoanza jana ni moja ya matayarisho ya kuanza kwa mradi huo katika kipindi cha mpito mwezi Oktoba mwaka huu.
Akifungua rasmi mafunzo hayo jana jijini Dar es Salaam, Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia aliwataka madereva hao kuyapokea kwa bidii na umakini mkubwa.
“Mafunzo haya yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa,” alisema wakati wa maadhimisho hayo katika eneo la Ubungo
Waziri Ghasia aliieleza kwamba mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani kwa mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na kuwa mafunzo hayo yatahusu pia namna ya kuhudumia wateja.
“Madereva hawa watajengewa weledi na nidhamu katika kazi yao ambayo kwa sasa inalalamikiwa sana na wananchi wakilalamikiwa kwa utovu wa nidhamu na kutotii sheria za barabarani,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiki alisema kuzinduliwa kwa mafunzo hayo ni ushahidi wa dhamira ya serikali kutatua kero ya usafiri na msongamano wa magari jijini humo kupitia mradi wa BRT.
“Mradi huu wa aina yake nchini na barani Afrika utatoa fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi ambayo ndio msingi wa maendeleo ya nchi,” alisema.
Mafunzo hayo kwa madereva wazalendo yanafanyika baada ya kushinda usaili ulio endeshwa na wataalamu kutoka chuo cha ufundi stadi na mafunzo (VETA).
Jumapili iliyopita kampuni ya watoa huduma wa ndani wa mradi huo, UDA-RT iliendesha semina ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na huduma za kipindi cha mpito za mradi huo.
Mradi huo wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa kilometa 20.9 za barabara maalum kutoka Kimara hadi Kivukoni; barabara ya Msimbazi kutoka Faya hadi Kariakoo-Gerezani na sehemu ya barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni hadi eneo la makutano ya Morocco.

Comments

Popular posts from this blog