Jokate: Wazazi wasiingilie mapenzi ya watoto
Brighton Masalu
SIKU chache baada ya gazeti dada
ya hili la Ijumaa Wikienda kuripoti juu ya wazazi wa Jokate Urban
Mwegelo ‘Kidoti’ kumkataa Ali Kiba kama mchumba wake, binti huyo
ameibuka na kuwataka wazazi kote nchini kuacha kuwaingilia watoto wao
katika masuala ya kimapenzi, akidai jambo hilo ni vema wakiachiwa
wenyewe.
Akizungumza
na gazeti hili, Jokate alisema ni vyema kama wazazi wakawaacha watoto
wao waoe au kuolewa na watu wawapendao, kwani vinginevyo ni kuwaingilia
maisha na uhuru wao binafsi, jambo ambalo si jema.
“Unajua
nimelala, madai ya Ally (Kiba), sitaki kuyazungumza sana, unajua mimi
ni binti mtu mzima, ninao uhuru wa kumchagua nimpendaye kwa ajili ya
maisha yangu, ifike mahali wazazi wawape uhuru watoto wa kufanya mambo
yao, awamu hii siko tayari kuona naumizwa tena na familia juu ya
uhusiano wangu,” alisema binti huyo kwa njia ya simu juzi.
Comments
Post a Comment