Asasambua mchana kweupe kumkomesha mchepuko
MUME
wa mtu sumu! Kitendo cha wanawake kutembea na waume za watu ni cha
kawaida kabisa katika maeneo mengi nchini na wengi wamejikuta wakikutana
na balaa, lakini tabia hiyo inaendelea kila kukicha. Samora Abdallah
(pichani), Afisa Mtendaji wa Mtongani, Kata ya Mbuyuni, Kinondoni jijini
Dar es Salaam, anao mkasa wa kusisimua ambao ni moja kati ya kesi
nyingi alizopata kuzifanyia kazi ofisini kwake kama anavyosimulia;
“Hata sijui nianzie wapi, kuna siku
kundi la watu walifika ofisini kwangu, nilipohoji ujio huo kwa kuwa
haukuwa wa amani, nikajibiwa kwa kuoneshwa kidole kwa dada mmoja
aliyeshukiwa kuchukua mume wa mwenzie. Mara wakaanza kurushiana maneno
machafu, nusura wakunjane, nikawazuia na kutaka kujua kulikoni.
“Dada mmoja akaniambia kuwa binti
aliyekuwa mbele yetu, anatembea na mumewe kwamba siku hiyo aliichukua
namba yake kutoka kwenye simu ya mume wake na kuanza kuchat naye
akijifanya ndiye yeye. Alizungumza naye mambo mengi na mwishowe akamtaka
aje sehemu wakutane, dada huyo bila kujua kuwa anaingia mtegoni,
akaenda.
“Baada ya kufika alipo, akakutana naye,
akamuuliza alichokifuata eneo hilo, huyo mwanadada akaanza kujiumauma,
akidai kuna mtu anamsubiri, basi akampigia simu yake, akasogea pembeni
ili akazungumze, huyo dada mwenye mume akakata simu, akamfuata na
kumzaba vibao, akimwambia yeye ndiye aliyempigia na kumuuliza kwa nini
anatembea na mume wake.
“Akasema watu waliwakuta wakizozana,
wakawashauri kuja ofisini kwangu, wakiwa hapa ndipo yule dada akaanza
kuvua nguo ili kati yao aonekane mzuri ni nani ndipo nilimzuia na
kumwambia kufanya vile ilikuwa ni kujidhalilisha, yule dada alimuomba
msamaha kwamba asingerudia kutoka na mumewe aliyemdanganya.
Kama una kituko kilichowahi kukutokea
ukiwa ofisini wasiliana nasi kupitia namba iliyopo hapo juu. Angalizo ni
lazima uwe Mwenyekiti, Mtendaji au Mjumbe wa Shina, Kijiji au Mtaa
Comments
Post a Comment