Posts

YEMI ATANGAZA SIKU YA KUZIKWA BABA YAKE.

Image
Baba yake Yemi Alade aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi, J.A. Alade enzi za uhai wake. MWANAMUZIKI wa kike wa Nigeria, Yemi Alade,  na familia yake watafanya  maziko ya marehemu baba yake tarehe 7 na 8 Mei mwaka huu. Baba yake Alade aliuyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi, J.A. Alade, alifariki  Januari 16 mwaka huu na binti yake huyo ambaye ni mtunzi wa wimbo maarufu wa ‘Johnny’, hajasema mengi kuhusiana na kifo hicho tangu kitokee. Mwanamziki wa kike wa Nigeria anayetamba kwa wimbo wa Jonny, Yemi Aladeakiwa katika pozi. Ni katika mahojiano ya gazeti la Tribune yaliyofanyika Machi 13, mwaka huu (siku ya kuzaliwa kwake) ndipo  aliposema maziko ya baba yake yatafanyika Mei 7 na 8. Yemi Alade ni mtoto wa mwisho kwa baba yake huyo kutoka kabila la Wayoruba na mama kutoka kabila la Waigbo.

MWANAFUNZI ATEKWA, AUAWA

Image
Na Waandishi Wetu DUNIA imekwisha jamani! Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mabibo, Dar, Irene Said (15) ametekwa, amebakwa na kuuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili huku ikidaiwa kuwa, kijana mmoja asiyejulikana alifika nyumbani kwao, Kigogo Luhanga na kutaka kiroba na mtu mmoja waongozane akabebe ndizi. Polisi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu. Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha sana, mama mdogo wa marehemu, Doto Lucas alisema:  “Siku ya tukio ambayo ni Alhamisi iliyopita (Machi 12), kijana mmoja ambaye hakuna aliyemfahamu alikuja hapa nyumbani na kumtaka mtu mmoja na kiroba ili akachukue ndizi ambazo kuna mtu aliagiza ziletwe. “Marehemu ndiye aliyekuwa karibu akijisomea baada ya kutoka shuleni. Mtu mkubwa aliyekuwa nyumbani muda huo ni bibi wa marehemu ambaye ni mtu mzima hivyo alimwambia Irene aongozane na mtu huyo akachukue mzigo akijua uk

MADAI: AK47 ALIPIGWA KABLA YA KIFO CHAKE

Image
Mwili wa AK47 ukitolewa katika mochwari ya Hospitali ya Nsambya. WAKATI wapenzi wa muziki nchini Uganda wakiwa bado wamegubikwa na simanzi kwa kuondokewa na mwanamuziki wa miondoko ya dancehall, Emmanuel Mayanja maarufu kwa jina la AK47, taarifa mpya zimeibuka kuwa kuna uwezekano kuwa alipigwa kabla ya kifo chake. Jose Chameleon (katikati) akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mdogo wake. AK47 amefariki dunia   usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali baada ya kuanguka akiwa bafuni. Taarifa hizo zinadai kuwa atakuwa alipigwa katika baa aliyokuwemo iitwayo Dejavu, iliyopo eneo la Kabalagala kabla ya kupelekwa Hospitali ya Nsambya, Kampala ambapo mauti yalimkuta. Baa hiyo inamilikiwa na Jeff Kiwanuka, aliyekuwa meneja wa wasanii wawili Radio na Weasel. Pallaso (mwenye tisheti ya bluu) ambaye naye ni kaka wa marehemu akifarijiwa na mwanamuziki Bebe Cool. Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kabalagala, Nusulah Kemigisha

MWANAFUNZI ATEKWA, AUAWA

Image
Polisi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu. DUNIA imekwisha jamani! Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mabibo, Dar, Irene Said (15) ametekwa, amebakwa na kuuawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili huku ikidaiwa kuwa, kijana mmoja asiyejulikana alifika nyumbani kwao, Kigogo Luhanga na kutaka kiroba na mtu mmoja waongozane akabebe ndizi. Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha sana, mama mdogo wa marehemu, Doto Lucas alisema: “Siku ya tukio ambayo ni Alhamisi iliyopita (Machi 12), kijana mmoja ambaye hakuna aliyemfahamu alikuja hapa nyumbani na kumtaka mtu mmoja na kiroba ili akachukue ndizi ambazo kuna mtu aliagiza ziletwe. “Marehemu ndiye aliyekuwa karibu akijisomea baada ya kutoka shuleni. Mtu mkubwa aliyekuwa nyumbani muda huo ni bibi wa marehemu ambaye ni mtu mzima hivyo alimwambia Irene aongozane na mtu huyo akachukue mzigo akijua uko jirani kwa mujibu wa mtu huyo. “Baada ya muda, yule kijana alirud

MAAJABU MAKUBWA DAR! MTOTO AZALIWA BILA UBONGO WA NYUMA!

Image
Mtoto anayedaiwa kuzaliwa bila ya ubongo wa nyuma(medulla oblongata).Na Haruni Sachawa NI maajabu! Mwanamke mmoja, Diana Dioniz mkazi wa Magomeni Makuti jijini Dar es Salaam, ameangua kilio cha kuomba msaada baada ya mtoto wake aliyezaliwa mwaka mmoja uliopita kugundulika kuwa hana ubongo wa nyuma (medulla oblongata), hali inayosababisha shingo kulegea na macho kutoona. Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake, Diana alisema alipata ujauzito wa mtoto huyo na kujikuta akiwa na furaha kubwa, lakini baada ya kuzaliwa na kumpa jina la John, amejikuta akipata mateso makubwa, kwani kwa muda wote, shingo yake inakuwa imelegea na macho yake hayaoni. “Majirani walinishauri nimpeleke hospitali kwa uangalizi zaidi, nilipomfikisha Muhimbili nikaambiwa suala la mwanangu linapaswa kushughulikiwa na daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Kitengo cha Moi,” alisema mwanamke huyo. Aliongeza kuwa, baada ya kupelekwa huko na kuchunguzwa ndipo ilipojulikana kuwa na matatizo hayo, ambay

DIAMOND NUSURA AKATWE MGUU! KWA UGONJWA WA KISAHANI

Image
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata wapi aliyewahi kuwa mchumba wa Wema Sepetu, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenusurika kukatwa mguu katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia ugonjwa wa Foot Corn (maarufu kwa jina la kisahani) kumtesa kwa kipindi kirefu. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Diamond ambaye kwa sasa anaminya kimalavidavi na mwanamama Zarina Hassan ‘Zari’, alianza kusumbuliwa na ugonjwa huo takribani siku 730 zilizopita (miaka miwili), huku mwenyewe akipuuzia matibabu yake na kuelekeza nguvu kwenye shoo za ndani na nje ya nchi. “Mara kwa mara alikuwa akilalamikia maumivu makali ya mguu lakini kwa kuwa yalikuwa yakija na kupotea, alikuwa akipuuzia kwenda hospitali mpaka juzi (Ijumaa) alipoamua kwenda TMJ,” kilisema chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa jina. WALICHOKIBAINI MADAKTARI “Madaktari walipompim

Haya ndiyo madhara ya kuitana 'Sweet, Dear, Baby' kwenye mapenzi

Image
BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby! Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine). Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji. HUTUMIKA WAPI HASA? “Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.” Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha pe

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI(NACTE)LINAKARIBISHA MAOMBI YA KUJIUNGA NA UALIMU 2015/2016

Image
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Makao makuu ya ofisi hizo  Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne  Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali  kama zinavyopatikana kwenye  tovuti ya baraza hilo: www.necte.go.tz.Waombaji  ; watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga  na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbali mbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.Kulia ni Katibu msaidizi wa Baraza hilo Ramadhani Samainda. Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari pichani katika Makao makuu ya ofisi hizo  zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, waka

SYLVESTRE MARSH AAGWA JIJINI DAR

Image
Padre akiongoza ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh. Waombolezaji wakifuatilia ibada ya kumuaga Marsh katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Michezo ya Championi, Saleh Ally akiaga mwili wa kocha Marsh. Wadau mbalimbali wakiuaga mwili wa Sylvestre Marsh. Mwili wa Marsh ukitolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mapaparazi wakichukua matukio wakati wa zoezi hilo. Mwili wa Marsh ukiwa tayari kupelekwa kwenye gari. ALIYEKUWA kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh, ameagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. Marsh aliyefariki dunia jana, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua maradhi ya saratani ya koo kwa muda mrefu. Awali alilazwa hapo akapata nafuu na kupelekwa kwao Mwanza, lakini wiki iliyopita alirudishwa tena na ndipo umauti ulipomku

ZITTO AKABIDHI AMBULANCEA JIMBONI KWAKE

Image
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana March 14 ametoa gari mpya ya kubebea wagonjwa (Ambulance)kama moja ya ahadi zake alipokuwa kwenye kampeni ambapo aliahidi kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi wake atatoa gari hiyo. Wakipokea msaada huo Michael Mwandezi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kigoma pamoja na Hamis Said Betese ambaye naye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Nyarubanda ambao ndio msaada huo wamemshukuru sana Mbunge Zitto Kabwe.  Hata hivyo kabla ya kuelekea kukabidhi Gari hiyo ya kubebea wagonjwa,Zitto Kabwe aliwatembelea Wanachama wa Chama cha Ushirika Rumaco ambao wanajishughulisha na kilimo cha Kahawa kutoka kijiji cha Matyazo Kigoma Kaskazini.  Hapa Zitto akiwa kwenye shamba lake la kahawa

KOCHA MARSH AFARIKI DUNIA

Image
Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh enzi za uhai wake. ALIYEKUWA kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh, amefariki dunia asubuhi ya leo. Marsh alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuungua maradhi ya saratani ya koo kwa muda mrefu, awali alilazwa hapo akapata nafuu na kupelekwa kwao Mwanza, lakini wiki iliyopita alirudishwa tena na ndipo umauti ulipomkuta. Sylvestre Marsh enzi za uhai wake akiwa na Kim Poulsen. Marsh ambaye aliwahi kuipa mafanikio makubwa klabu ya Kagera Sugar, amewahi kufundisha soka kwa mafanikio makubwa sana hapa nchini kuanzia mwaka 2003, alipokuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana, chini ya Abdallah Kibadeni. Mwaka 2006, alipandishwa timu ya wakubwa na kuwa kocha msaidizi chini ya Mbrazil Marcio Maximo na baadaye akawa chini ya Wadenish, Kim Poulsen na Jan Poulsen. Hata hivyo, tangu mwaka jana kocha huyo

PAPA FRANCIS ATOA ISHARA ZA KUJIUZULU

Image
Papa Francis na alyiekuwa papa Benedict Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amedokeza kwamba huenda akafuata nyayo za mtangulizi wake Papa Benedict kwa kujiuzulu.Akihojiwa na runinga moja ya nchini Mexico katika sherehe za maadhamisho yake ya pili tangu achaguliwe,Papa Francis amesema kuwa anahisi kwamba uongozi wake katika kanisa hilo hautaendelea kwa kipindi kirefu. Amesema kuwa hatua ya Benedict kujiuzulu mwaka 2013 ni ya ujasiri na haifai kuchukuliwa kama ya kipekee.Papa Benedict ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kujiuzulu tangu papa Gregory wa 12 mwaka 1415. Papa Francis anasema kuwa anatamani maisha yake ya kuwa muhubiri na angependelea kuzuru maeneo kadhaa bila kujulikana. CHANZO BBC

SIMBA SC WAICHAPA MTIBWA SUGAR BAO 1-0 TAIFA,OKWI AWAPA RAHA

Image
Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Okwi leo baada ya kufunga bao pekee la ushindi dakika za lala salama dhidi ya Mtibwa Sugar Na Mahmoud Zubeiry BAO la Emmanuel Anord Okwi dakika ya 90 ushei limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Simba SC sasa inafikisha pointi 29 baada ya mechi 18 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 30 za mechi 16 sawa na vinara Yanga SC, wenye pointi 31. Okwi alifunga bao hilo, wakati tayari baadhi ya wapenzi wa Simba SC wameanza kutoka uwanjani, wakiamni matokeo ni sare.  Mganda huyo, alifunga baada ya kupata pasi ya Abdi Banda na kumchambua vizuri kipa aliyefanya kazi nzuri leo, Said Mohamed Kasarama. Emmenuel Okwi akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Said Mkopi katika mchezo wa leo Beki wa Simba SC, Hassan Kessy akimtoka kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi  Mch