HAPENDWI MTU INAPENDWA POCHI...JANGA LINALOVUNJA NDOA!
NImatumaini yangu wapenzi wasomaji wa safu hii mko poa na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika siku ya leo na kuweza kuperuzi ukurasa huu muhimu wa kuzungumzia masuala ya uhusiano. Leo napenda nizungumze nanyi kuhusu mada iliyopo hapo juu. Kwa uchunguzi mdogo nilioufanya, inaonekana ndoa zilizofungwa miaka ya 80 kurudi nyuma zilikuwa na uhai mrefu kuliko miaka ya juu ya hapo. Ndoa miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikisuasua, hazina umri mrefu. Watu wanaingia kwenye ndoa kwa kufuata kitu flani mbele ya safari kikitoweka, hayupo tayari kuvumilia, unakuwa ugomvi na ndoa kuvunjika. Wazee wetu walifunga ndoa kwa kufuata misingi ya ndoa. Kigezo cha fedha hakikupewa nafasi kubwa katika mapenzi, walitazama zaidi suala la maisha ya kusaidiana na matakwa ya Mungu katika sheria za ndoa. Mume alijua wajibu wake kama baba wa familia lakini mke pia alijua wajibu wake ndani ya familia. Kila mmoja alifuata kiapo alichokula siku ya ndo