KUNDI LA PANYA ROAD LATIKISA DAR JANA
KIKUNDI kinachodaiwa kuwa Panya Road kimetikisa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi. Maeneo yaliyokumbwa na dhooruba hiyo ni pamoja na Sinza, Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo usiku huu. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundimakundi. Imeelezwa kuwa fujo zilianzia mchana leo baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye Diamond kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga . Baada ya kumzika mwenzao leo, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo. Usiku ulipoingia wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar. Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo baa. Wateja waliokuwa