Zari The Bosslady na Diamond Platnumz ni KIMYE wa Afrika!


Kabla ya kukutana na Diamond Platnumz, Zari the Bosslady alikuwa tayari ni mwanamke maarufu nchini Uganda. 
Utajiri na urembo wake ulimfanya aitwe Kim Kardashian wa Uganda.
Zari anamiliki msululu wa magari ya kifahari yakiwemo Range Rovers, Bentley, Limousine, Mercedes Benz, Chrysler na mengine ambapo mengi kati yake yana plate number za jina lake.
Anamiliki mijengo kibao pamoja na biashara mbalimbali kikiwemo chuo kikubwa kilichopo nchini Afrika Kusini.
Kukutana na Diamond Platnumz ambaye ukubwa wake tunaufahamu, umemfanya msichana huyo mwenye watoto watatu kuwa na nguvu zaidi na ndio maana couple yao inaweza kufananishwa na ya Kanye West na Kim Kardashian.
Kama ilivyo kwa Kimye, Zari na Diamond wana sumaku ya skendo.
Ni hivi juzi tu mkanda wa ngono wa Zari ulisambaa mtandaoni ambao uliisha kulikuza tu jina na umaarufu wake.
Kwa sasa wawili hao wameanza kuongozana kama kumbikumbi. Baada ya kumsindikiza Diamond kwenye tuzo za Channel O kisha kuwa pamoja kwenye ‘Ciroc All White Party’ jijini Kampala, wawili hao wapo pamoja tena kwenye ziara ya Diamond ya Burundi na Rwanda.

Kwa ukubwa wao kila mmoja, wawili hawa sasa ni miongoni mwa couple zenye nguvu zaidi katika burudani barani Afrika.

Comments

Popular posts from this blog