Posts

LORI LA MAFUTA LARIPUKA MBEYA...INAHISIWA DEREVA ALISINZIA

Image
Lori la kusafirisha mafuta likiwa na shehena kubwa ya mafuta aina ya Diesel limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali ya kugongwa na lori lingine katika eneo la igurusi wilayani mbarali.  Ajali hiyo imetokea  ikihusisha lori lenye namba za usajili t 417 ABF, mali ya kampuni ya Camel oil ambalo lilikuwa likisafirisha lita 35,000 za mafuta aina ya diesel kutoka jijini Dar es salaam kwenda nchini Congo DRC ambalo linadaiwa kugongwa na lori lingine. Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia ajali hiyo  wameitaka serikali kuwalazimisha wamiliki wa malori kuhakikisha magari yao yanakuwa na madereva wa akiba kwa kuwa wanaamini kuwa ajali hiyo imesababishwa na dereva wa lori moja wapo kusinzia wakati akiendesha gari kutokana na uchovu wa safari ndefu. Mpaka napata hizi habari hizi na chanzo kinatoka katika hilo la ajali, bado lori hilo lilikuwa likiendelea kuteketea huku kukiwa hakuna msaada wowote wa kuuzima moto huo.

BIBI KIZEE AZUA TAFRANI JIJINI MWANZA.......NI BAADA YA KUDAI AMEANGUKA KUTOKA ANGANI AKIWA NA WENZAKE BAADA YA KUGOMBANA WAKAMDONDOSHA.

Image
Kila mtu alikuwa na lake kuhusu bibi huyu anayedaiwa kukutwa akiwa uchi huku wengine wakisema ni mgonjwa wa akili na wengine wakidai ni mchawi kaanguka na ungo. Alipokuwa akihojiwa amedai ametoka Bariadi lakini wenzie aliokuwa nao walimshusha baada ya kutokea ugomvi. Amedai walikuwa wanne kwenye safari yao hata hivyo wapo wengine waliosema kuwa ni mgonjwa akili na tangu jana amekuwa akionekana maeneo ya hospitali ya sekoutoure akiranda randa. Mpaka naondoka eneo hilo Polisi walikuwa wamefika ili kutoa msaada kutokana na kundi la watu waliokuwa wamemzunguka na baadhi yao wakitaka apigwe kwa madai ni mchawi. Hapa chini ni baadhi ya picha zake. Akiongea huku akichorachora chini.  Akihojiwa na watu Hapa muda mchache baada ya kukutwa na Camera ya Kijukuu blog. Kundi la watu wakimshangaa bibi

NEWS ALERT: PATASHIKA MLIMANI CITY LEO BAADA YA MALL HIYO KUPIGWA BEI KWA NAKUMAT...!!!!

Image
  Makundi makubwa ya watu  yanaonekana yametapakaa katika shopping mall ya Mlimani City jijini Dar es salaam leo baada ya mall hiyo kuuzwa kwa mmiliki mwingine inayesemekana kuwa ni NAKUMAT. Hapo ni wafanyakazi wa Mlimani City wakisubiri hatma yao. Habari zaidi tunafuatilia.

BIFU LA WEMA NA KAJALA LAMALIZIKA, WEMA ATANGAZA RASMI KUPITIA AKAUNTI YAKE

Image
Wemasepetu  Good morning instagramers.... Hope you all well... If y'all must know mimi ni mtu ambaye huwa nasomaga sana comments.... Na kama nimekosa kusoma comment yako ujue ni kwamba zinakuwa nyingi mno na nashindwa soma zote.... Ni kwa muda mrefu sana mnaniona nakaa tu kimya na sisemi chochote khs my friendship life... But mimi binafsi na muhusika ndo tunajua... saa nyingine mnaongea hadi nakereka but nakaa kimya... Nilitaka tu kusema mimi sina kinyongo na mtu... na kama kuisha mbona yalishaisha...Au ndo mlikuwa mnataka kuona bega kwa bega...? In my life siwekagi vinyongo... nyi wenyewe mnajua... So jus so u want to know hayo yalishapita na maisha yanaendelea... ni hayo tu... Have a good day everebadi.. But chakushangaza Mlimbwende huyo wa Tanzania wa mwaka 2006 hakuweza kuweka picha ya shostito wake huyo kwenye hiyo post badala yake akaweka picha ya Shostito wake wa sasa Aunty Ezekiel ndio aliepamba post hiyo. Mmmmh je hapo unalionaje hilo? mdau.

ANGALIA PICHA BRAZIL WAKIIADHIBU CROATIA

Image
Neymar akishangilia bao lake la kwanza. Neymar akitupia bao la pili kwa mkwaju wa penalti. Marcelo (wa pili kulia) akijifunga na kuwapa bao la kuongoza Croatia katika dakika ya 11. Oscar baada ya kufanya hitimisho. WACHEZAJI Neymar na Oscar wamepeleka vilio Croatia baada ya kuipa ushindi wa mabao matatu timu yao ya Brazil kwenye mechi ya ufunguzi wa Fainali za Kombe la Dunia 2014 zinazofanyika nchini Brazil. Croatia walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 11 ambalo ni la kujifunga likiwekwa kimiani na beki Marcelo wa Brazil. Baadaye wenyeji Brazil walikuja juu na kusawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji wao mahiri anayefananishwa na Pele, Neymar kwa shuti la mbali lililomuacha mlinda mlango wa Croatia, Stipe Pletikosa katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili Neymar aliipatia Brazil bao la pili kwa mkwaju wa penalti ambao kipa Pletikosa alijaribu kuupangua lakini ukajaa wavuni na kuwapa wenyeji ushindi wa 2-1 dakika ya 71. 

PICHA ZA JENNIFER LOPEZ NA PITBULL WALIVYONOGESHA UFUNGUZI WA KOMBE LA DUNIA 2014 NCHINI BRAZIL

Image

MWANAMKE MWINGINE TENA ABAKWA HADI KUFA NA MWILI WAKE KUNING'INIZWA JUU YA MTI

Image
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 19 amekutwa amening’inizwa juu ya mti katika kijiji kimoja Kaskazini mwa India, likiwa ni tukio la tatu kutokea ndani ya wiki moja katika Jimbo la Uttar Pradesh. Mwili wa mwanamke huyo umekutwa katika eneo la Moradabad ambapo familia yake imewaambia polisi kuwa alibakwa huku uchunguzi wa madaktari ukiendelea kufanyika.Mwanamke mwingine alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika Jimbo la Uttar Pradesh siku ya Jumatano.Mwezi uliopita mabinti wawili wadogo walibakwa na kundi la watu katika mazingira kama hayo na kuibua maandamano ya hisia kali nchini India. Siku ya Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 nae alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika eneo la Bahraich.   Polisi wamesema kuwa alikuwa akipatiwa vitisho na wanakijiji kwa kuuza pombe katika eneo hilo na familia yake ilifungulia kesi watu watano kuhusiana na kifo hicho.

HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2014/2015

Image
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (MB) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2014/15 . UTANGULIZI  1.Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2014/2015. Pamoja na hotuba hii, nimewasilisha vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina takwimu za Bajeti. Kitabu cha Kwanza ni makisio ya mapato; Kitabu chaPili ni makisio ya matumizi ya kawaida kwa wizara, idara za Serikali zinazojitegemea, wakala na taasisi za Serikali;  Kitabu cha Tatu ni makisio ya matumizi ya kawaida kwa mikoa na mamlaka za serikali za mitaa; na Kitabu cha Nne ni makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa wizara, idara za Serikali zinazojitegemea, wakala na taasisi za Serikali, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa.  Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2014 ambao ni sehemu ya bajeti hii. <<BOFYA  HAPA  KUISOMA  HOTUBA  HIYO>> AU &

BREAKING NEWS: Chelsea ime msajili cesc Fabregas

Image
SHARE PICTURE           +10 Blue: Cesc Fabregas has signed for Chelsea from Barcelona on a five-year deal +10 New signing: Fabregas will wear the No 4 shirt and counts as a homegrown player for Chelsea +10 Make it official: Barcelona released an official statement thanking Fabregas for his time +10 Feud: Fabregas (right) has had several run-ins with Chelsea's players in the past +10 Raring to go: Fabregas and Spain face Holland on Friday night in their World Cup opener

KIJANA ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUKUTWA AKITAKA KUMLAWITI KIJANA MDOGO ENEO LA RADIO ARUSHA

Image
Kijana mmoja muda huu ambaye jina lake halijafahamika Mara moja amekutwa Bila aibu Akimlawiti mtoto wa miaka 12 maeneo ya PPF Njiro.  Tukio zaidi tazama hapa chini  Amani Athumani aliyembaka Mtoto wa Miaka 12 muda mchache uliopita Huyu ndiye dogo ambaye amelawitiwa ana umri wa Miaka 12.  Amani Athumani akiwa Chini ya ulinzi baada ya kukamatwa akiwa anamlawiti kijana wa Miaka 12  Mashuhuda wakiwa wanamshangaa kijana huyo aliyebaka  Wananchi wenye Hasira kali wakiwa  wanataka kuanza kumtandika kijana huyo... Mpaka sasa kijana huyo yupo eneo alililo kamatwa Njiro karibu na PPF.  Picha na Arusha yetu Blog

MISS IRINGA KUFANYIKA JUNI 20

Image
Baadhi ya washiriki wa redds miss iringa wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mazoezi katika ukumbi wanakofanyia mazoezi hotel ya Gentle Hill iliyoko mkoani Iringa.  Na Denis Mlowe,Iringa   HATIMAYE kinyang’anyiro cha kumsaka Redds Miss Iringa kinatarajia kufanyika Juni 20 mwaka huu baada ya aliyekuwa mratibu wa kwanza Mohamed Mcholeka kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kushindwa kufanyika Juni 6 kama lilivyopangwa mwanzoni na Tanzania Daima kuwa la kwanza kuripoti kuhusiana kutoweka kwa shindano hilo.   Waandaji wa Redds Miss Tanzania chini ya Lino Agency Hashim Lundenga baaada ya kugundua hilo wamempatia kibali cha kuandaa shindano hilo ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa tasnia ya urembo na kwasasa Redds Miss Iringa imepata mratibu mwingine ambaye ni kutoka kampuni ya Chakudika Intertainment chini uongozi wake Victor Chakudika ambaye ni Meneja wa kituo cha radio ya Nuru Fm ya mjini Iringa.   Akizungumza na Tanzani

MWONEKANO WA SOKO LA KARUME ULIVYO BAADA YA KUUNGUA NA MOTO JANA

Image

SOMA JINSI WANAWAKE WANAVYO-SHAMBULIWA NA U.T.I

Image
U.T.I  kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia  mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra) Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection. Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja  pindi mgonjwa anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo. Kuna wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama  normal flora na huwa ni askari wa mwili. Vijidudu hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa  haja kubwa na kuenea mpaka sehemu za s

MAJAMBAZI WAVAMIA KITUO CHA POLISI KIMANZICHANA NA KUUA ASKARI

Image
Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.  Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30. Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia. Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeru