JE, WAJUA WAPENZI WANATAKIWA WAKUTANE KIMWILI MARA NGAPI KWA WIKI, ILI KURIDHISHA NAFSI ZAO?
Kwa wiki nzima nimekuwa nakusanya mawazo, kutoka kwa wapenzi mbali mbali ambao walikuwa wananisaidia uchunguzi wangu juu ya namna wanavyoshiriki tendo la ndoa na kulidhika. Wengi kati ya hao kwa kiwango tofauti cha kuanzia mara tatu na kuendelea waliniambia kuwa hawatosheki na viwango hivyo na kuliacha swali kubaki kuwa wapenzi wakutane mara ngapi kwa wiki ili watosheke? Jibu la swali hili linapatikana baada ya kutambua kitu kimoja muhimu, nacho ni chanzo cha kutosheka hasa nini? Katika hali ya kawaida kutosheka kupo zaidi akilini na wala si mwilini, hii ina maana kwamba watu wanaodhani kuupa mwili mahitaji zaidi kadiri unavyodai ni njia ya kuutosheleza wanajidanganya, kwa sababu tamaa ya mwili haitoki mwilini bali kwenye akili ya mtu. Kwa msingi huo mtu akitaka kutosheka na penzi la mpenzi wake, ni lazima kwanza aitosheleze akili yake na kile anachopata, zoezi ambalo atalifikia kwa kutathimini uwezo wake wa kufanya mapenzi na wa mp