Rais wa Comoro Awasili Zanzibar Kuhudhuria Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi

  Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa DR. Ikililou Dhoinine akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar na Kupokea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa Dr. Ikililou Dhoinine akisalimiana na baadhi ya wana jumuiya ya Wakfi ya Wangazija hapa Zanzibar waliofika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Kumpokea.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa DR. Ikililou Dhoinine  kwenye chumba cha watu mashuhuri(VIP)hapo uwanja wa ndege wa Zanzibar.Picha na Hassan Issa-Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Comments

Popular posts from this blog