TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI DAR ES SALAAM NOVEMBER 11, 2013. Jeshi la Polisi nchini linapenda kuutaarifu umma kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Robert Manumba amefikia umri wa kustaafu kisheria ambao ni miaka sitini (60) katika utendani wake wa kazi. Aidha, katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka (1976 – 1977), mwendesha mashtaka wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, 1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo cha polisi Dar es salaam, (1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Magomeni na Kinondoni na Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam (1987 – 1993), Pia, amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Arusha, ( 1993 – 1995), Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi ( 1995 – 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi, (1996 – 1997), Mkuu wa kitengo cha usalama wa nchi, intelijensi