Posts

Msikiti wa Answar Sunna ulipo mjini DODOMA wateketea kwa moto mchana huu.

Image
Msikiti mkubwa wa  Answar Sunna  uliopo  barabara ya saba mjini Dodoma  umewaka  moto  mchana  huu  ikiwa  ni  muda  mfupi  baada  ya  swala  ya  mchana  kumalizika.... Akiongea  kwa  njia  ya  simu  na  Mpekuzi wetu, mmoja  wa  mashuhuda  walioshuhudia  tukio  hilo  amedai  kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  moto wa  JIKO  la  wakazi  wa    ghorofa ya  juu  ya  jengo  la  msikiti  huo... Hata  hivyo, shuhuda  mwingine  aliyeongea  na  mtandao  huu  amedai    kuwa  chanzo  cha  moto  huo  ni  hitilafu  ya  umeme  iliyoanzia  ghorofa  ya  juu  ya  jengo  hilo.   Kwa  mujibu  wa  mashuhu...

Picha tano za yule daktari FEKI aliyenaswa katika hospitali ya KCMC

Image
      Daktari feki aliyenaswa katika hosptali ya KCMC aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo. Daktari Feki akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa 'akihudumia'. Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo (kushoto) akimwonesha Daktari Feki, Alex Massawe. Daktari Feki akiwa katika gari la polisi tayari kupelekwa kituoni. Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, jana ulimnasa 'Daktari Feki' aitwaye Alex Sumni Massawe (33). Massawe alikamatwa saa 5:00 asubuhi ndani ya hospitali hiyo na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amepanga kumfanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa malipo ya Sh. 200,000. Habari zin...

Daz Baba achanganyikiwa na kuwa KICHAA... wadau wasema ni Bangi na Madawa ya kulevya

Image
Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure Namba 8′ Daz Baba amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu. Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii wenzake. Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia  mwandishi wetu  jana akiwa mkoani Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili zote za mtu ambaye  ni  Kichaa na amekuwa mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya matukio ya ajabu. “Hivi juzi juzi Daz alienda nyumbani kwa Afande usiku, akapiga kelele sana, Afande akaamka na kumkuta Daz akiwa mchafu na akiongea maneno ambayo hayaeleweki, baadaye alitaka kumfanyia tendo baya kwa mfanyakazi wa kike wa Afande lakini hakufanikiwa, ila watu wakajua kweli Daz hayuko sawa,” alisema. Baada ya taarifa hiy...

Ripoti maalumu ya gazeti la MWANANCHI kuhusu vurugu zilizotokea jana bungeni

Image
  Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake. Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti. Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo. Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi...

Polisi na Mawaziri wadaiwa kujihusisha na biashara haramu ya NGONO

Image
BAADHI ya mawaziri na polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao, maarufu kwa jina la Changudoa. Hayo yameelezwa jana na Jukwaa la Wanaharakati Wanawake Vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo jijini Dar es Salam. Wanaharakati hao wanawake vijana, walisema tatizo liko kwenye jamii ambayo inawahukumu changudoa bila kujiuliza kuwa wateja wao ni kina nani. ‘’… jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja wake nani? Kwa taarifa yako, mawaziri, wabunge na mapolisi wamo; na hii ni changamoto kwa jamii,’’ walisema wanaharakati hao.   Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kutoka jukwaani, kiongozi wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, alisema wameamua kutoa ujumbe huo kwa washiriki wa tamasha hilo ili jamii ijue wateja wa changudoa hao. Alisema wateja hao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza m...

Video ya ngono ya wabongo yavuja.....Ni siku chache baada ya ile ya Mrisho Ngasa kunaswa

Image
Baada  ya  video  ya  ngono  ya  Mrisho  Ngasa  kuvuja  na  kusambaa  kwa  kasi, video  nyingine  ya  wabongo  imevuja  wakifanya  uchafu  wao  huku  wakijirekodi..... <<VIDEO  IKO  HAPA,  BOFYA  HAPA>>

Hali ya msanii Banza Stone ni mbaya

Image
NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ameanza kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani. Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wetu, Banza alisema alipomaliza shoo ya Sikukuu ya Iddi na Bendi ya Extra Bongo, alianza kuugua, akaenda Hospitali ya Yemen iliyopo Sinza, Dar ikagundulika ana malaria kali ambapo alipewa dozi ya siku saba. “Nilipewa dawa za malaria nikameza nikaambiwa baada ya siku saba nitajisikia vizuri lakini mpaka sasa sioni mabadiliko yoyote, bado mwili unaniuma sana, nashinda kitandani kila siku hivyo muziki basi kwa sasa,” alisema Banza na kuongeza:   “Najua mashabiki wangu watanimisi lakini kwa sasa muziki nimepumzika, naomba mashabiki waniombee.”

Hatimaye mshindi wa Big Brother afanikiwa kumpata baba yake ( Ni yuleyule aliyemkana )

Image
Hatimaye teknolojia imefanikisha kuwakutanisha wazazi wa mshindi wa Big Brother Afrika ‘The Chase’ Dillish Mathews baada ya mwanaume mmoja aitwaye Abdi Galgayo Guyo kuja hadharani na kudai kuwa ni baba mzazi wa mshindi huyo wa The Chase. Siku moja tu iliyopita, Pulse iliandika habari kuhusu mwanaume wa Kenya aitwaye Abdi Galgayo Guyo aliyetembelea ofisi za Standard Media ya Kenya na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa mshindi wa BBA Th Chase.  Abdi ambaye kwa mujibu wa Standard ana asili ya Somalia alielezea jinsi alivyokutana na mama yake Dillish aitwaye Selma kati ya (April 1989) na (March 1990) alipoenda Namibia akiwa mmoja wa maaskari wa Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopelekwa nchini humo kusimamia amani.   Habari hizo zilipokelewa kwa hisia tofauti na watu mbalimbali ambao wengi wao walionekana kuamini kuwa Abdi anazusha ili apate pesa, na Dillish alivunja ukimya kwa kutweet akimshangaa mwanaume huyo na kusema baba yake ...

MAANDAMANO YA KUMKUMBUKA MAREHEMU MWANGOSI MKOANI IRINGA

Image
Katibu wa IPC Francis Godwin akiongoza maandamano ya wanahabari na wadau huku akiwa juu ya gari na picha ya marehemu Daud Mwangosi. Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari mkoa wa Iringa ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi yakipita eneo ya Uhindini. Wanahabari Iringa katika maandamano ya kumuenzi marehemu Mwangosi jana. Wanahabari wa vyombo mbalimbali na wadau wa habari mkoa wa Iringa wakiwa katika maandamano ya amani ya kumuenzi aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC). Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari yakipita eneo la soko kuu la manispaa ya Iringa.   Wananchi wakishuhudia maandamano hayo. Katibu Mtendaji wa IPC, Francis Godwin akitoa taarifa ya kuanza kwa maandamano ya kumuenzi marehemu Daud Mwangosi jana. Katibu wa IPC Francis Godwin (kushoto) akikabidhi picha ya marehemu Daud Mwangosi kwa Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard (kulia), wanaoshuhudia ni Mzee Fulgence Malangalil...

WAZIRI WA UJENZI DKT.MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA UCHUKUZI WA MALAWI

Image
Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt. John Magufuli (kushoto) leo amekutana na Waziri wa Uchukuzi kutoka Malawi Mh.Sidik Mia (wapili pichani kutoka kulia) pamoja na Ujumbe wake jijini Dar es Salaam.Pichani( katikati) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Herbet Mrango. Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt. John Magufuli (kushoto) akiongea na Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mh. Sidik Mia(kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam(katikati) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hebert Mrango. Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt, John Magufuli (alienyanyua mkono) akiongea na ujumbe kutoka Malawi alipokutana nao leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam Waziri waUjenzi Mh. Dkt. john Magufuli (kushoto) akimkabidhi nyaraka Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mh. Sidik Mia (kulia) leo jinini Dar es Salaam,walipokutana na kuzungumza masuala mbalimbali yakiwemo kuimarisha ushirikiano katika nyaja za usafirishaji .(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango. Waz...

KISIWA CHA SAANANE HIFADHI MPYA YA TAIFA

Image
Kisiwa cha Saanane kimetangazwa rasmi kuwa Hifadhi ya Taifa kufuatia Tangazo la Serikali Namba 227 lililotolewa hivi karibuni. Kutangazwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kunafuatia kupitishwa kwa Azimio la Bunge mwezi Oktoba mwaka jana lililoridhia kupandishwa hadhi kwa kisiwa hicho kutoka Pori la Akiba na kuwa Hifadhi ya Taifa. Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane itakuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 2.18 na itajumuisha maeneo ya lililokuwa Pori la Akiba , Visiwa vya Chankende kubwa na ndogo pamoja na eneo la maji ya Ziwa Victoria linalozunguka visiwa hivyo. Kuanzishwa kwa Hifadhi mpya ya Taifa ya Saanane kutawezesha haja ya kuongeza spishi mbalimbali za wanyamapori na hivyo kuongeza utalii wa mjini, utalii wa ndani, utafiti na kutoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi na wananchi watakaotembelea hifadhi hii mpya. Aidha, uamuzi huu utasaidia kutunza hali ya bioanuwai, uhifadhi wa mazalia na makuzio ya samaki n...

NHIF YAZINDUA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA YA JAMII (CHF)MJINI KILWA

Image
Adoh Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akipokea vifaa maalum vya kuhifadhia fedha na nyaraka mbalimbali kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa uzinduzi wa Huduma za Bimaya Afya (CHF)katika halmashauri hiyo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Mkapa Garden Mjini Kilwa, wa pili kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Kaimu Mkurugenzi wa (NHIF) Khamis Mdee na kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani na Fortunata Raymond Msimamizi wa NHIF mkoani Lindi.wananchi mbalimbali wakiwemo wazee walijitokeza katika zoezi la upimaji wa afya yakiwemo magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la Damu ikiwani pamoja na kupima Uzito Urefu. Ado Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za Bima ya Afya katika Halmashauri ya wilaya ya Kilwa jana kulia ni Bw. Khamis Mdee Kaimu Mkurugenzi NHIF na kushoto ni Dr. Hilda Mwakipesile kutoka NHIF. ...

OZIL ATUA ARSENAL, FELLAINI AKIJIUNGA NA MAN UTD

Image
Lukas Podolski (kulia) na Mesut Ozil (kushoto) katika pozi na jezi ya Arsenal nchini Ujerumani. Mshambuliaji mpya wa Man Utd, Marouane Fellaini (kushoto) akikabidhiwa jezi na kocha wake David Moyes (kulia). Marouane Fellaini ndani ya Manchester United. -OZIL ATUA KWA KITITA CHA BILIONI  107, FELLAINI BILIONI 69.3 KLABU ya Arsenal imefanikiwa kumnasa kiungo wa Ujerumani, Mesuit Ozil kwa ada ya pauni milioni 42.5 sawa na bilioni 107 za Tanzania. Usajili wa Ozil umevunja rekodi katika klabu hiyo inayoongozwa na Mfaransa Arsene Wenger. Staa huyo wa Ujerumani aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano na atakuwa akilipwa  pauni 140,000 sawa na milioni 352.8 za Tanzania kwa wiki. Wakati Arsenal wakimnasa Ozil katika dakika za mwisho za dirisha la usajili kufungwa, Manchester United wao wamefanikiwa kumnasa Mshambuliaji wa Everton, Marouane Fellaini kwa ada ya pauni milioni 27.5 sawa na bilioni 69.3 za Tanzania. Fellaini ameungana na kocha wake wa zamani David Moye...

MSANII WA KIZAZI KIPYA AFUNGWA JAELA MIEZI 21 BAADA YA KUWATUKANA POLISI

Image
Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tunisia amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa kuwatusi polisi , miezi miwili tu baada ya kuachiliwa kufuatia maandamano ya umma. Ala Yaacoubi, anayesifika kwa jina Weld El 15, alifungwa jela miaka miwili mnamo mwezi Juni kwa kutoa wimbo uliokuwa unawafananisha polisi na Mbwa ambao unasema kuwa polisi wanapaswa kunyongwa. Hata hivyo hukumu yake iliondolewa mwezi Julai alipoachiliwa ingawa inadaiwa kuwa aliendelea kuimba wimbo huo. Hukumu hii imetolewa wakati yeye mwenyewe hakuwa mahakamani na kwa hivyo atahitajika kujikabidhi kwa polisi. Wakili wake anasema kuwa kesi hiyo ilihusu zaidi kushambulia uhuru wa watu kujieleza. "nitazungumza na mteja wangu kupinga uamuzi huu , lakini hukumu zinazotolewa dhidi ya wasanii zinaonyesha kuwa vita dhidi ya...

MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA TAMASHA LA 11 LA TGNP JIJINI DAR ES SALAAM YAFANA

Image
Tamasha la 11 la mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) limeanza kwa maandamano katika ofisi za TGNP eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam. Maandamano hayo yameanzia lango kuu la ofisi za TGNP na kuhitimishwa katika viwanja vya tamasha eneo hilo la TGNP. Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo mkurugenzi wa TGNP Usu Mallya alisema wakati TGNP inaazimisha tamasha hilo bado inajivunia mapambano makubwa yaliyodumu kwa miaka 16 katika kupigania jengo hilo ambalo lilikuwa na kesi mahakamani hadi wanaposhinda kesi hiyo. Hivyo alisema ushindi wa kesi hiyo dhidi ya jengo hilo utawafanya sasa kuendelea kuboresha zaidi jengop hilo na kulifanya kuwa la kisasa zaidi na kuendeleza mafunzo mbali mbali. Chanzo:Francisgodwinblog