Daz Baba achanganyikiwa na kuwa KICHAA... wadau wasema ni Bangi na Madawa ya kulevya



Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure Namba 8′ Daz Baba amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu.

Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii wenzake.

Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia  mwandishi wetu  jana akiwa mkoani Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili zote za mtu ambaye  ni  Kichaa na amekuwa mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya matukio ya ajabu.

“Hivi juzi juzi Daz alienda nyumbani kwa Afande usiku, akapiga kelele sana, Afande akaamka na kumkuta Daz akiwa mchafu na akiongea maneno ambayo hayaeleweki, baadaye alitaka kumfanyia tendo baya kwa mfanyakazi wa kike wa Afande lakini hakufanikiwa, ila watu wakajua kweli Daz hayuko sawa,” alisema.

Baada ya taarifa hiyo mwandishi wetu  alimtafuta Afande Sele, ndipo alipothibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema ameshampatia taarifa dada yake Daz wa Dar es salaam.

“Kweli hali ya Daz ni mbaya sana nimejaribu kumuweka sawa lakini nimeshindwa labda wakamfanyie matambiko ya kwao kwasababu baba na mama yake walifariki na walikuwa hawaelewani labda kuna matatizo ya kifamilia.” alisema Afande.

Comments

Popular posts from this blog