Posts

Nimepewa majina ya wabunge wauza dawa za kulevya: Wamo CCM, Chadema

Image
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, amesema amepokea majina ya wabunge, viongozi wa serikali na wafanyabiashara maarufu nchini ambao ni mapapa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Hata hivyo, Dk. Kigwangallah ambaye amepania kuwataja bungeni watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, amesema baada ya kukabidhiwa majina hayo kutoka kwa wananchi, anafanya uchunguzi na kupata ushahidi ili kujiridhisha kabla hajachukua hatua ya kuwataja. Miongoni mwa majina ya wabunge aliyopewa wamo kutoka CCM na Chadema, na wafanyabiashara maarufu wote wanatoka mkoa wa Dar es Salaam. "Nawashukru wananchi wamenipa ushirikiano hadi jana wamenikabidhi majina ya watu saba ambao ni wabunge wawili, kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali na wafanyabiashara wanne, ambao wote ni mapapa wauza unga na siyo madagaa," alisema Dk. Kingwangallah. Alisema katika kuhakikisha anatekeleza alichoahidi amemwandikia barua Spika wa Bunge kumuomba atoe maelezo

Kumbukumbu Ya Kuawa Kwa Mwangosi Na Swali La Mtoto Yule...

Image
Ndugu zangu, HUWEZI kutawala miili ya watu ukaacha mioyo yao. Ndiyo, mjumbe hauawi, ni kauli ya hekima ya tangu enzi za wahenga wetu. Leo ni mwaka mmoja tangu mwandishi wa habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa, Daud Mwangosi kuawa. Ilikuwa ni Jumapili ya Septemba 2, 2012. Hakika, siku ile itabaki katika kumbukumbu za Watanzania kwa mamilioni. Ni kwa kufikiwa na taarifa za kutisha za mauaji ya mwandishi wa habari. Haya yanaingia katika historia kuwa ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi wa habari kufanyika hadharani tangu nchi hii ipate Uhuru. Wengi watakuja kukumbuka walikuwa wapi na walifanya nini siku walipopata taarifa hizo za kutisha. Binafsi, taarifa ile ya mauaji ya Daud Mwangosi siku ile ya Jumapili ya huzuni kwa Taifa ilinikuta nikiwa Iringa Mjini. N umbali wa mwendo wa saa moja kwa gari kufika eneo la tukio, Nyololo, Mufindi. Jioni ile nilikuwa nikifundisha soka ya watoto. Mara baada ya kupata taarifa zile kwa simu, nili

MAHAFALI YA KWANZA IRINGA RETCO BUSINESS COLLEGE

Image
Mh Jaji mstaafu Raymond Mwaikasu akimtunuku Cheti cha Astashahada na Stashahada ya uongozi wa Biashara pamoja na tuzo ya uanafunzi Bora 2010 Beatrice Ndekwa. Wasanii wa kikundi cha Ngoma toka Mkwawa Magic Site wakitumbuiza, 

Waliopanda mbegu DECI hatarini kutolipwa

Image
WATEJA wa Kampuni ya DECI waliopanda mbegu, wanaweza wasilipwe fedha zao, MTANZANIA Jumatatu limebaini. Wateja hao ambao wanaidai kampuni hiyo Sh bilioni 39.27, huenda wasilipwe fedha zao kwa kuwa mchezo wa upatu hautambuliki kisheria. Utata huo ulijulikana mwishoni mwa wiki, baada ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, kuzungumza na MTANZANIA Jumatatu. "Kwanza kabisa, niseme tu kwamba hadi sasa hatujapata nakala ya hukumu hiyo ili kujua inatuelekeza nini kuhusu mchakato wa kuwalipa hao waliopanda mbegu. "Tukipata hukumu hiyo, ndiyo tutaisoma na kufahamu tumepewa jukumu gani na gharama zitalipwa na nani katika kutekeleza mchakato huo. "Sisi tunataka tujue hiyo hukumu inamaanisha nini, maana kwa kawaida anayechezesha na anayecheza upatu wote wana makosa, sasa utamlipaje aliyecheza? "Lakini, kwa kuwa hatujaiona hiyo hukumu, hatujui imetuelekeza nini, lakini i

LAPF KUTUMIA BILIONI 35 UJENZI WA KITUO CHA MABASI MSAMVU

Image
Na Fatma Salum na Hassan Silayo- MAELEZO Mfuko wa pensheni wa LAPF unatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 35 katika mradi wa kituo cha mabasi eneo la msamvu Mkoani Morogoro. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa mfuko huo Kanda ya Mashariki Sayi Lulyalya alisema mradi huo ambao ni ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na mfuko wa LAPF unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu. Sayi alisema hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo ambao utakamilika baada ya miezi 18 zimeshaanza kwa kuzungushia uzio katika eneo la ujenzi wa kituo hicho. "LAPF imeamua kutenga takriban bilioni 35 za ujenzi wa kituo cha Msamvu na tunashukuru uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwa kutoa eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na michoro imeshakamilika na shughuli za zabuni zinaendelea." Alisema Sayi. Aidha Sayi aliongeza kuwa mradi huo wa uwekezaji utahusisha ujenzi wa hoteli yenye

DIAMOND ATUHUMIWA KUIBA WIMBO WA DYNA..."MY NUMBER ONE"

Image
 Baada ya tuhuma za kuiba wimbo wa H.Baba na Pasha,Msanii Naseeb Abdul Diamond Platnum, ameingia tena ndani ya tuhuma nzito  baada ya  madai   kwamba wimbo anaotaka kuuachia wa No.1 ni wa Dayna. Inasemekana awali Dayna alimtaka Diamond wakafanye wimbo kwa Shedy, Diamond akakubali, akaskiliza mdundo na kumuahidi Dayna kwamba wangefanya wote. Lakini baadae Diamond akamrubuni Shedy na kumwambia ile bit ampe na aachane na kazi ya Dayna. Hii ni demo ya wimbo wa Dayna ambao unafanana kila kitu na wimbo wa Diamond anaotaka kuachia.

MWANAUME ANYWESHWA VIROBA NA "KULIWA JICHO" ( KABAANG) BAADA YA KULEWA

Image
JESHI la Polisi mkoani Singida linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni katika manispaa hiyo kwa tuhuma za kumlawiti mwenzake na kumharibu vibaya sehemu za haja kubwa baada ya kumnunulia pombe kali aina ya viroba jogoo tisa.   Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya Kindai, na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Athuman.   Alisema kuwa baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, kijana aliyelawitiwa (jina tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa amelewa kupindukia na hivyo kila mmoja arejee nyumbani kwao.   “Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia mtuhumiwa amwache hapo ili apumzike kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana lakini ghafla alianguka chini na kisha na kupoteza fahamu,” alisema.   Baada ya muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile.   Alisema kuwa

CHADEMA WAMKANA AFANDE SELE....WADAI HAWAJAWAHI MUOMBA AGOMBEE UBUNGE MOROGORO..!!

Image
Gazeti la Habari Leo la siku ya leo tarehe 2 Septemba lenye kichwa cha habari "Chadema kuzoa wasanii mastaa" pamoja na mambo mengine, mwandishi amemnukuu mmoja wa wasanii toka mkoa wa Morogoro akisema amewahi kuombwa na viongozi wa mkoa wa CHADEMA kugombea Ubunge. NAOMBA KUWEKA KUMBUKUMBU SAHIHI. 1. Mimi ndiye mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Morogoro, ninayeongo za Baraza la Uongoz la mkoa lenye wajumbe wa5 tu tangu mwaka 2009. 2. Katika vikao vyetu vyote hukujawahi kuwepo kwa AGENDA ya kumuomba/ kumshawishi mtu yeyote kugombea nafasi yoyote. 3. Hatujawahi kumuomba Afande Sele kugombea. Mbali na hilo hatujawahi hata kumuomba tu kujiunga na CHADEMA.     4. Kwa upande wa gazeti la Habari leo, naungana na kauli ya JB kwamba, kuna dalili za wazi kwamba habari hii imepikwa na mwandishi mwenyewe. Asanteni Makamanda. PUUZENI TAARIFA HII Susan Limbweni Kiwanga

NELSON MANDELA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI

Image
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95), jana aliondolewa hospitali na kurejeshwa nyumbani ambako ataendelea na matibabu ya maradhi ya mapafu.  Hata hivyo, taarifa ya Serikali ya Afrika Kusini imesema uamuzi huo hauna maana kwamba Mandela amepata nafuu kwa vile hali yake bado ni mbaya na wakati mwingine hudorora zaidi. Taarifa hiyo imeongeza timu ya madaktari wa Mandela inaamini ataendelea kupata matibabu katika makazi yake mjini Houghton kwa kiwango sawa na anayopata akiwa hospitalini mjini Pretoria. Tangazo hilo limekuja siku moja tu baada ya maofisa wa serikali kukanusha ripoti kuwa shujaa huyo wa taifa hilo, alisharuhusiwa. Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel aliyekuwa amelazwa hospitali tangu Juni 8, mwaka huu anaheshimiwa duniani kwa kuongoza mapambano dhidi ya utawala wa kibaguzi wa wazungu wachache na kuhubiri upatanisho na maridhiano na jamii za weupe pamoja na kufungwa miaka 27 jela. “Timu ya madaktari imetuhakikishia kuwa Mandela ata

BREAKING NEWS: NDEGE ZAGONGANA ZANZIBAR.

Image
Ndege ya Oman air na Ethipian airlines leo jioni zimegongana katika kiwanja cha ndege cha Zanzibar wakati zikijitaarisha kuruka, ila ajali hii haikuwa kubwa, wakati hayo yakiendelea abiria wa Ehiopian airline wameshushwa na kuweka sehemu ya mapumziko. Nawatakia kila la kheri wasafiri wote na inshaalah Mwenyezi  Mungu atawapa wepesi wa katika safari zao. Ndege ya kulia ni ya Ethiopian airlines mayo ndiyo imeivaa Oman air hadi bawa kutoka source http://www.jestina-george.com

PICHA; YALIYOJIRI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA...!!

Image
Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza kwa wingi katika kumuanga SHUJAA WA INJILI Dr Moses Kulola aliyefariki 29 Agosti saa 5.30 hapa jiji Dar. Kati ya watu ambao wamekuwepo katika ibada hii ya kuuaga mwili wa Dr Askofu Moses Kuloa, wamehuduria watumishi wa Mungu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maaskofu wainjilisti mitume na manabii. Askofu kulola alizaliwa mkoani Mwanza, mwaka 1930 na kufariki 29 agost 2013. Baadhi ya watumishi Katika uhai wake mzee Kulola alifanya kazi ya Injili hadi kifo kinamchukuwa, ila kati ya kazi aliyoifanya ni pamoja na kutembea kwa mguu kutoka Mza hadi Mtwara. Lakini pia safari nyingi alizozifanya zilikuwa katika mazingira magumu. Amehubiri injili ndani na nje ya nchi. Mama Kulola (Mjane Mtoto wa Mzee Kulola Willy, akilia kwa uchungu   Askofu Silvester Gamanywa akimpa pole mama Kulola Watumishi wa Mungu mbalimbali wakisubiria mwili wa Dr Moses Kulola Msafara wa mwili wa marehemu D

SISTER FEKI ANASWA NCHINI KENYA

Image
Sister feki baada ya kunaswa akikusanya fedha. ..Akipekuliwa mabegi… POLISI mjini Narok nchini Kenya wanamshikiria mwanamke mmoja aliyenaswa akiwa na mavazi ya kitawa akikusanya fedha kutoka kwa watu wenye mapenzi mema akidanganya kuwa ni sister. Mwanamke huyo alikuwa akikusanya misaada ili aweze kurudi katika konventi alipotokea mpaka hapo aliposhutukiwa kuwa hakuwa mtawa. Alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vitambulisho kadhaa. Mpaka ananaswa, sister huyo alikuwa amewatapeli watu kadhaa na anatarajiwa kufikishwa mbele ya sheria kesho.  Habari / Picha: KTN

Obama ataka bunge liamue kuhusu Syria;

Image
Kwa muda wa zaidi ya wiki sasa , Ikulu ya Marekani ya White House imekuwa ikielekeza mashambulizi yake kuelekea kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria. Lakini hayo yamebadilika rais Obama anataka sasa bunge liamue. Uamuzi wa Rais Barack Obama wa ghafla badala yake wa kuomba ruhusa ya bunge unamuweka katika hatari ambayo inaweza kuharibu hali yake ya kuaminika iwapo hakuna hatua itakayochukuliwa kujibu shambulio la silaha za kemikali ambalo limekiuka kile binafsi alichosema kuwa ni kuvuka "mstari mwekundu". Bunge la Marekani halijatatua karibu chochote cha maana tangu mwaka 2010, likishindwa kukamilisha kile ambacho hapo kabla kilikuwa wajibu wa msingi kwa masuala ya barabara , shule , mashamba na masuala ya mawasiliano nchini Marekani. Kuomba ruhusa ya baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican pamoja na baraza la seneti linalodhibitiwa na chama chak

MWANAMKE HUYU ADHAMIRIA KUWEKA REKODI YA DUNIA KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAUME 100,000 DUNIANI KOTE....!!

Image
Mwanamke mmoja raia wa Poland ameripotiwa kuweka nadhiri ya kusafiri katika kila mji duniani katika uchunguzi usio wa kawaida kulala na wanaume 100,000. Ania Lisewska kutoka mjini Warsaw ameingia katika mpango huo usio wa kawaida kwenye mji aliozaliwa mwezi uliopita na mpaka sasa amefanikiwa kuongeza idadi hiyo kufikia 284, kwa mujibu wa gazeti la Huffington Post. Lakini wakati rafiki yake wa kiume wa muda mrefu mwenye umri wa miaka 21 akimsamehe zaidi kuliko wote - hajamtosa pamoja na yote hayo - anaeleweka kwamba 'hajasisimuliwa' na wazo hilo. Ania alisema kwamba rafiki yake huyo amelazimika 'kukubaliana na wazo hilo'. Alilieleza gazeti la Austrian Times: "Nataka wanaume kutoka Poland, Europe na duniani kote. Ninapenda ngono, kufurahi na wanaume. "Nchini Poland somo la ngono bado ni haramu na yeyote anayetaka kukidhi matakwa yao ya ngono huchukuliwa kama aliyepotoka, au mgonjwa wa akili.&q

MAMBO YAKUZINGATIA KWA WANAWAKE WANAO TAKA KUOLEWA

Image
Hata kama utapingana na mimi, lakini ukweli utabaki pale pale; Kila jinsia inahitaji sana kuungana na jinsia nyingine katika tendo muhimu na la kihistoria katika maisha liitwalo ndoa! Yes, huu ni ukweli ambao upo wazi na utaendelea kusimama kama ulivyo. Jinsia zote zina umuhimu na jambo hili muhimu, lakini kuna tofauti kidogo, kwamba mwanamke  anasubiri kufuatwa na mwanaume, wakati mwanaume anaamua kumfuata mwanamke anayemtaka na kwa wakati wake. Kuna kitu nataka kuweka sawa hapa, kwamba wanaume ndiyo huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume husika. Wanawake wa ‘mjini’ huwa hawakubaliani na hili, kutokana na huu utandawazi unaohubiriwa siku hizi ikiwa ni pamoja na kampeni za usawa zinazotetewa na Wanaharakati Wanawake. Akina dada nao huchangamkia kueleza hisia zao kwa wanaume. Nadhani si jambo baya, ingawa linaweza kupokelewa kwa hi

UVCCM LAMUIDHINI​SHA SIXTUS MAPUNDA KUWA KATIBU MKUU MPYA

Image
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akifungua Mkutano maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo, katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mjini Zanzibar. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Zanzibar), Shaka Abdul Shaka, Katibu Mkuu wa UVCCM aliyemaliza muda wake, Martine Shigela na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.

Mwili wa Askari aliyefariki kwenye Mapigano Congo Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo Wawasili nakuzikwa Zanzibar.

Image
Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, aliyefarika Nchini Congo, akiwa katika Jeshi la Kulinda Amani.  Ndege iliobeba Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar ikitokea Dar-es-Salaam.  Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijumuika na Ndugu na Jamaa kuupokea mwili wa marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo.ulipowasili Zanzibar kwa mazishi Kijijin kwao Fujoni kwa mazishi jioni hii.  Ofisa wa JWTZ akitowa maelezo ya ratiba ya kuupokea Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo katika uwanja wa ndege wa Zanziba leo mchana na kuzikwa katika Kijiji cha Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.  Mjane wa Marehemu na Watoto wake wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume leo mchana wakitokea Mjini Dar-es- Salaam.  WANAJESHI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa n