VIJANA sita waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Kyela mkoani Mbeya wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kyela kujibu mashtaka manne wanayokabiliana kutokana na vurugu walizozifanya msikitini, ambapo Shekhe Mkuu wa Wilaya Kyela, Nuhu Mwafi lango na waumini wengine walipigwa na kuumizwa.Tukio hilo lilitokea wakati wa Sikukuu ya Idiel- Fitr, wakati shekhe huyo akiongozwa swala. Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kyela, Joseph Luambano, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Nicholaus Tiba kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa manne. Ilidaiwa kuwa kosa la kwanza ni kula njama za kutenda kosa, kufanya vurugu msikitini, kufanya shambulio la kudhuru mwili na kujeruhi. Alidai kuwa siku ya tukio Shekhe Mkuu wa wilaya alishambuliwa akiwa anaendesha swala ambapo katika tukio hilo watu wengine, akiwemo mtunza hazina wa msikiti, Hamisi Hussein, alijeruhiwa kichwani. Aliwataja wat...