WANAOTUHUMIWA KUMPIGA SHEKHE WATINGA KORTINI.
- Get link
- X
- Other Apps
Ilidaiwa kuwa kosa la kwanza ni kula njama za kutenda kosa, kufanya vurugu msikitini, kufanya shambulio la kudhuru mwili na kujeruhi. Alidai kuwa siku ya tukio Shekhe Mkuu wa wilaya alishambuliwa akiwa anaendesha swala ambapo katika tukio hilo watu wengine, akiwemo mtunza hazina wa msikiti, Hamisi Hussein, alijeruhiwa kichwani.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ibrahimu shaban (17), Ambokile Mwangosi (19), Sadick Abudul (28), Mashaka Kassimu (30), Ahmed Kassimu (35 ) na Issa Juma (37). Alidai kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa hayo. Watuhumiwa wote walikana mashtaka wanayokabiliana nayo na upande wa mashtaka uliomba mahakama hiyo isiwapatie dhamana watuhumiwa ili wasivuruge ushahidi. Watuhumiwa walirudishwa rumande hadi hapo kesi yao itakapotajwa tena Agosti 26, mwaka huu ambapo shauri lao litasikilizwa tena
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment