MBOWE AWATAKA WANANCHI KUCHANGIA RASIMU YA KATIBA MPYA

Wananchi wa mkoa wa Mara wametakiwa kuchangia kikamilifu katika rasimu ya Katiba mpya ili wamuenzi Baba wa Taifa Mwl JULIUS KAMBARAGE NYERERE kupitia michango yao itakayoiwezesha Tanzania kupata Katiba mpya.
Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) FREEMAN MBOWE amesema mjini Musoma kuwa  suala la katiba ni jambo linalogusa maisha ya watanzania hivyo ni muhimu kutumia busara kujadili kwa mustakabali wa taifa.
Akizungumza katika mikutano na wananchi iliyofanyika kwenye wilaya za Bunda, Serengeti, Tarime na Musoma mjini MBOWE amempongeza Rais wa Tanzania Dk. JAKAYA KIKWETE kwa kukubali kuanzisha mchakato wa katiba mpya.
Kwa upande wake mbunge wa Ubungo JOHN MNYIKA aliyeambatana na Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mara kushiriki katika hatua zote zilizosalia katika kupata Katiba mpya ili wawe sehemu ya kuandikwa kwa historia 

Comments

Popular posts from this blog