CCM BADO INA IMANI KUBWA NA TUME YA KATIBA
Nape Nnauye NA MWANDISHI WETU CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimesema bado kina imani na Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya. Imesema licha ya CCM kutofautiana kimawazo katika baadhi ya maeneo katika rasimu ya kwanza ya katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini haina ugomvi na tume hiyo. Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. "Tunawaheshimu sana wajumbe wa tume hii, na kwa kweli tunamatumaini nao sana kuwa watatimiza wajibu wao kwa weledi mkubwa", alisema Nape. Nape alibainisha kwamba pamoja na maeneo mengine ya rasimu ya kwanza ya katiba , CCM ina mawazo tofauti kwenye suala la Muundo wa Muungano ambapo wakati rasimu inapendekeza muundo wa serikali tatu, CCM yenyewe inapende