CCM BADO INA IMANI KUBWA NA TUME YA KATIBA
- Get link
- X
- Other Apps
Nape NnauyeNA MWANDISHI WETU |
CHAMA CHA
MAPINDUZI (CCM) kimesema bado kina imani na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba nchini, katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya.
Imesema
licha ya CCM kutofautiana kimawazo katika baadhi ya maeneo katika rasimu
ya kwanza ya katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
lakini haina ugomvi na tume hiyo.
Hayo
yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi
Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
"Tunawaheshimu sana wajumbe wa tume hii, na kwa kweli tunamatumaini
nao sana kuwa watatimiza wajibu wao kwa weledi mkubwa", alisema Nape.
Nape alibainisha kwamba pamoja na maeneo mengine ya rasimu ya kwanza
ya katiba , CCM ina mawazo tofauti kwenye suala la Muundo wa Muungano
ambapo wakati rasimu inapendekeza muundo wa serikali tatu, CCM yenyewe
inapendekeza serikali mbili.
"Kama mnavyoona katika hili, wakati tume inapendekeza muundo wa
serikali tatu sisi CCM tunapendekeza muundo wa serikali mbili, lakini
hii haitufanyi tuwapuuze au tugombane na wale wenye mawazo tofauti na
yetu", alisema Nape na kuongeza;
"Kumekuwepo na ripoti na makala kadhaa zinazojaribu kuonyesha kama
vile kuna mvutano kati ya tume na CCM, au CCM na wengine wenye mawazo
tofauti na CCM. Ukweli ni kuwa hali hiyo inayojaribu kujengwa kwa nguvu
si ya kweli. Tuache hoja zishindane kwa hoja na nguvu ya hoja ndio iwe
msingi wa ushindani".
Nape alitaka ushindani uwe kwenye hoja bila kushutumiana ili jatimaye mawazo ya wengi yasikilizwe na kuzingatiwa.
Alisema, CCM inasisitiza kuwa itaheshimu mawazo ya Watanzania, kwani
katiba inayotengenezwa ni ya watanzania wote bila ya kujali itikadi zao.
"Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote wanaounga mkono
baadhi ya hoja za CCM hasa hoja ya serikali mbili. Tumeshuhudia maoni ya
wajumbe wengi wa mabaraza na wananchi kwa ujumla wakiunga mkono mawazo
haya ya CCM ya muundo wa muungano wa serikali mbili na hoja kadhaa
zingine", alisema Nape na kuongeza;
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment