Posts

MAMILIONI YA PESA ALIYOINGIZA DIAMOND KWENYE SHOW ZA MWEZI ULIOPITA ....

Image
  Staa wa Kesho, Diamond ameendelea kupiga hela kwa show nyingi zinazomfuata kila kukicha. Wingi wa show hizi unazidi kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye pesa nyingi zaidi. Tumejaribu kuangalia baadhi ya show alizofanya mwezi huu, atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao ili kukadiria ni kiasi gani anaweza kuwa ameingiza. Baadhi ya show tunafahamu ni kiasi gani aliingiza huku zingine tukikadiria kutokana na jinsi anavyochaji.   Show ya nchini Comoro 22 June Katika show hii alisema alilipwa si chini ya dola 25,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 38.   Show za Usiku wa wasafi Tabora 28 na 29 June Mara nyingi katika show za ndani Diamond hachukui si chini ya shilingi milioni 10 kwa show mbili huenda akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 15. Show ya Tigo Mwanza 30 June Katika show za makampuni kama hizi Diamond hulipwa si chini ya shilingi milioni 10.   Kili Music Tour 2013 Tulipata taarifa

GEORGE BUSH AMESHAANZA KAZI YAKE ILIYOMLETA... ...MKUTANO WA WAKE WA MARAIS UMEFUNGULIWA NA RAIS KIKWETE

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura na Mama Salma Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Wageni wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.  PICHA NA IKULU

RAISI GEORGE BUSH ALIPOKUTANA NA RAIS OBAMA TANZANIA KABLA HAJAONDOKA

Image
  Rais Obama pamoja na Rais Bush walikutana leo Asubuhi katika Ubalozi wa Marekani uliopo jijini Dar es Salaam na kufanya tendo la kutoa heshima zao kwa Walipoteza Maisha pamoja na wale wote walioathirika katika shambulio la Ugaidi katika Ubalozi wao hapa nchini mwaka 1998.

KWA HERI BARACK ABAMA....KARIBU TENA NA SAFARI NJEMA

Image
Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana.... Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo.... Tunapenda  kuungana na  Rais Jakaya  Kikwete na  watanzania  wote  wapenda amani katika  kumshukuru Rais wa Marekani Barack Obama kwa  kuichagua  Tanzania... Pia tunawapongeza  watanzania  wote kwa kuonyesha umoja  wetu na hata  kuzika itikadi zetu za kisiasa   na   hata  kupelekea  TV zaidi ya 1000 duniani na radio zaidi ya  3000 duniani  kuitazama  Tanzania..

MAHAKAMA YAWATIA MBARONI WAPENZI WAWILI WALIOAMUA KUTALII WAKIWA UCHI

Image
Njemba moja, Stephen Gough aliyewahi kuwa mwanajeshi amekamatwa na polisi katika Jiji la Portsmouth, Uingereza baada  ya kukutwa na mpenzi wake wakidunda kutalii mitaani wakiwa uchi wa nyama. Mwanamke Melodine Roberts aliyefuatana naye aliachiwa na polisi kwa kuwa mara baada ya kuonywa kuacha tabia hiyo, aliacha lakini mpenzi wake huyo aligoma na hii ni mara ya 14 akifanya hivyo licha ya kufungwa jela huko nyuma.   Baada ya kugoma polisi walimfunga pingu na wakampeleka mahakamani moja kwa moja  ambapo Mwendesha Mashitaka, Simon Jones alisema Gough alikuwa amekiuka sheria na aliwahi kufungwa miaka sita na moja ya makosa yaliyosababisha  afungwe ni kutemba uchi wa mnyama hadharani.   Baada ya maelezo hayo, jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Sarah Munro alisema kuwa kwenda jela kwa mtu huyo ndiyo ilikuwa njia pekee kwake kwa kuwa hilo ni kosa kubwa katika jamii ya Waingereza na ni ukiukwaji wa taratibu za umma wa sehemu hiyo.   Gough alikiri kosa hilo na hakujit

PICHA ZA MAMIA YA WANANCHI TOKA UBUNGO WAKISUBIRI MSAFARA WA RAIS OBAMA

Image

HUU NDIO UMATI WA WATU ULIOJITOKEZA ASUBUHI KATIKA BARABARA ALIYOPITA OBAMA KWENDA UBUNGO

Image

MKE WA OBAMA ATEMBELEA WAMA FOUNDATION NA KUKUTANA NA MAMA SALMA KIKWETE JIONI HII

Image
Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA  jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa  WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo... Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wako  katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Tanzania wakiongozana  na watoto wao jioni hii .... Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine.   Mama Mchelle Obama akielekea katika lango kuu la ofisi za WAMA jioni hii.   Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.   >Mama Michelle Obama akipozi kwa picha na mwenyeji wake mama Salma Kikwete    Wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya kumpokea Mama Michelle Obama   Mama Anna Mka

TRENI YA MWAKYEMBE ILIPATA AJALI JANA ASUBUHI ....HIVYO HUDUMA ZA TRENI ZIKAHAIRISHWA

Image
  Leo mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili vya treni ya huduma la jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam , katika jali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo wake alinusurika. Hata hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali ambapo viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya reli eneo la Kamata. Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika basi hilo la daladala ambapo majeruhi  wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbil wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli  mmojawapo akiwa  mahututi.   Vichwa hivyo viifanikiwa kufika stehesheni kwa wakati na kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini  kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya leo  jioni Julai 01, 2013, imesogezwa mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasi

MFALME MSWATI WA SWAZILAND AAONDOKA NCHINI NA AMEWATAKA WATANZANIA WABADILIKE

Image
Mfalme Mswati wa Swaziland akisindikizwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kurejea nyumbani baada ya kufungua maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere Julai 1,2013. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na mfalme Mswati wa Swaziland ambaye aliondoka nchini baada ya kufungua maonyesho ya Kiataifa ya Biashara kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)   ---------   MFALME Mswati (III) wa Swaziland amewataka Watanzania kubadilika kwenda sambamba na Soko la Pamoja la Afrika Mashariki kwa kubuni bidhaa mbalimbali zenye ubora.    Alisema watanzania pia wanapaswa kuzipa kipaumbele bidhaa zinazozalishwa nchini kwa lengo la kushindana katika biashara duniani. Mswati aliyasema hayo jana wakati akifungua Maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, barab

JE WAJUA SIFA ZA GARI ANALOTEMBELEA RAISI OBAMA - THE BEAST

Image
BONYEZA PICHA YA CHINI ILI KUWEZA KUSOMA MAANDISHI KWA UKUBWA  Picha ya pili inaelezea kila kitu katika gari hiyo

MMILIKI WA FACEBOOK NA WAFANYAKAZI WAKE WASHEREHEKEA KUPITISHWA KWA SHERIA YA NDOA YA JINSIA MOJA

Image
Mmiliki wa mtandao wa kijamii Facebook CEO Mark Zuckerberg amejiunga na wafanyakazi wa kampuni yake waliozidi 700 katika matembezi ya kusherekea maamuzi ya mahakama kuhusu haki za ndoa ya jinsia moja. Matembezi haya yamefanyika mitaa ya San Francisco Jumapili Asubuh. Sheria hio inayo sherekewa Imeruhusu wanandoa wa jinsia moja kumiliki leseni ya ndoa ndani ya siku 30 baada ya kuoana. 

HUU NDO MWONEKANO MPYA WA AGNESS MASOGANGE,HAKIKA AMETOKELEZEA MBAYAA

Image
Baadhi ya Picha chache Mpya za Agness Masogange ....Hizi amezitupia kwenye Instragram yake .

MAKAMU WA RAIS KENYA ADAI KENYA INA MARAFIKI WENGI TOFAUTI NA MAREKANI NA KAMWE HAWAWEZI KURUHUSU SERA YA USHOGA YA OBAMA

Image
NAIBU wa Rais Bw William Ruto, jana alivunja kimya chake kuhusu hatua ya rais wa Marekani Barack Obama kutozuru humu nchini kwa kusema hatua hiyo haina madhara yoyote kwa Kenya. Huku akiongea katika kanisa la Katoliki la St Gabriel Bahati, kaunti ya Nakuru,  Bw Ruto alisema nchi hii ina 'marafiki’ wengine wengi duniani ambao inaweza kushirikiana nao huku akiongezea kuwa hatua ya rais Obama kukwepa kutembelea Kenya haiwezi kutatiza kwa vyovyote vile uhusiano mwema uliopo wa kibiashara baina ya Marekani na Kenya. “Tunaiheshimu nchi ya Marekani nayo inafaa kuwaheshimu Wakenya,” akasema Bw Ruto. Alisema serikali tayari imeanzisha mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na mataifa  mengine  huku akikariri kuwa  safari ya Rais Uhuru Kenyatta nchini Uganda ambapo alikutana na rais wa nchi hiyo Yoweri  Museveni na mwenzao wa Rwanda rais Paul Kagame kujadili jinsi nchi hizo tatu zinaweza kushirikiana kibiashara, ni miongoni mwa mi

MATUKIO YA RAIS BARACK OBAMA AKIWASILI NCHINI MCHANA HUU, TAZAMA PICHA ZA KILA KILICHOJIRI AIRPORT

Image
Rais Barack Obama wa Nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba na watoto wao, wakiwasili mchana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku mbili hapa nchini. Ndege ya Raisi wa Marekani Ikiwa Kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mgeni wake wa Marekani, Barack Obama aliewasili nchini Mchana huu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Rais Barack Obama akikagua Gwaride maalum aliloandaliwa akiongozwa na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenelari Davies Mwamunyange. Rais barack Obama akiagana na mama Salma Kikwete Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere. Msafara wa Viaongozi ukiondoka Uwanja wa Ndege. Picha zote kwa Hisani ya TBC1 TOA MAONI YAKO HAPA CHIN

PICHA ZA RAIS OBAMA ALIPOTUA KATIKA ARDHI YA TANZANIA

Image
 Rais Baraka Obama akicheza ngoma alipokua akipita kwenye moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbuiza kwa ajli ya ujio wake mara tu aliposhuka kutoka kwenye ndege ya Airforce One  Mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete akitabasamu wakati mgeni wake Rais Barack Obama alipokua akitikisa mwili kwa hisia za ngoma za asili zilizokua zikitumbuizwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa ujio wake leo akitokea Afrika ya Kusini.  Rais Barack Obama akiangalia moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbuiza uwanjani hapo.  Rais Barack Obama akikagua majeshi ya ulinzi na usalama. Rais wa Marekani Barack Obama pamoja mkwewe wakilakiwa na mwenyeji wao Rais Jakaya Kikwete mara tu walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere leo Jumatatu July 1, 2013 kwa ziara ya siku 2., kushoto ni mama Salma Kikwete.   Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama akipokewa kwa Shangwe Ikulu, Dar es