TRENI YA MWAKYEMBE ILIPATA AJALI JANA ASUBUHI ....HIVYO HUDUMA ZA TRENI ZIKAHAIRISHWA
Leo mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili vya treni ya huduma la jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam , katika jali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo wake alinusurika.
Hata
hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali ambapo
viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya
reli eneo la Kamata. Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika
basi hilo la daladala ambapo majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbil wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli
mmojawapo akiwa mahututi.
Vichwa hivyo viifanikiwa kufika stehesheni kwa wakati na kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya leo jioni Julai 01, 2013, imesogezwa mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasiri.
mabadiliko haya yamebidi yafanyike kufuatia Jiji la Dar es Salaam kuwa na hekaheka ya kumpokea Raisi wa Marekani Barack Obama.
Aidha uongozi wa TRL unawataarifu wakazi wa jiji kuwa kesho Julai 02, 2013, huduma za treni ya jiji hazitakuwepo hadi keshokutwa Julai 03, 2013, ambapo zitaendelea kama kawaida.
Imtolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.
Makao Makuu ya TRL
Dar es Salaam.
Julai 01, 2013.
Comments
Post a Comment