NGONO KINYUME NA MAUMBILE ZAONGEZEKA TANZANIA ....WENGI WAO WANAFANYA KUONDOA MIKOSI
Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Nchini (Tacaids) imesema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa vitendo vya ngono kinyume na maumbile vinazidi kuongezeka. Hayo yalisemwa jana na Dk. William Kafura, katika mkutano wa sita wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (Tapac). Alisema hiyo inatokana na imani za kishirikina kwamba wakifanya vitendo hivyo watapata bahati kwa kupandishwa vyeo. “Lazima tukubali tatizo lipo na tulitafutie suluhisho, utafiti upo umefanywa na Muhimbili, umefanywa na chuo kikuu cha Dar es Salaam, umefanywa na Tasisi ya Utafiti ya Ifakara,” alisema. Alisema pia wafanyabiashara wanaamini kwa kufanya vitendo hivyo watajirika wakati wanawake wanaamini kuwa watazidi kupendwa. Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho, alisema utafiti uliofanyika nchini unabainisha kuwa wanawake hawana uelewa wa kutosha juu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi. Akizungumzia suala la kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi Dk. Mrisho alisema kuwa wanaume wana uelewa