FAMILIA YA NGWEA YAMKATAA MTOTO WAKE ALIYELETWA NA MAMA YAKE MAKABURINI
Siku chache baada ya aliyekuwa mkali wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth
Mangweha ‘Ngwea’ kupumzishwa kaburini kufuatia kifo cha usingizini
nchini Afrika Kusini kilichotokea Mei 28, mwaka huu, mambo kibao
yanazidi kuibuka.
Mtoto wa Ngwea akiwa na baadhi ya wanafamilia wakati wa mazishi ya baba yake.
Habari zinadai kuwa familia ya marehemu Ngwea
imemkataa mtoto aliyeletwa na mama yake makaburini akidaiwa kuwa ni
mtoto wa Ngwea.
Juni 6, mwaka huu wakati wa mazishi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alitimba akiwa na mtoto huyo wa kike aitwaye Neema Albert na kudai kuwa alimzaa na Ngwea mwaka 2001, wakati msanii huyo akisoma Sekondari ya Mazengo.
Wakati akijieleza, ndugu wa Ngwea, Anthony Mangweha alikuwa akimsikiliza ambapo aliwataja wanandugu wa marehemu waliokuwa wakijua suala hilo.
Waliotajwa kujua kuwa mtoto huyo alikuwa wa Ngwea ni Frank, Jotam na Amani ambao waliwahi kutumwa na marehemu kwenda kumwangalia mkoani Dodoma.
Hata hivyo, ndugu huyo aliyekuwa akimsikiliza alimtaka mama Neema kupoa, hadi familia ikae kikao.

“Kweli wikiendi iliyopita familia ilikaa kikao kwa zaidi ya saa 7,
pamoja na mambo mengine lakini wanadaiwa kufikia uamuzi mzito wa
kumkataa mtoto huyo hadi mama Neema apeleke vigezo vya uthibitisho,”
kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.
Akizungumzia suala hilo
kwa sharti la kutotajwa , mmoja wa dada zake Ngwea alisema: “Ni
kweli yule mtoto aliondoka na mama yake lakini kama akileta uthibitisho
tutampokea.”
Comments
Post a Comment