WAKENYA WALIVYOANDAMANA JUNE 11 NA KINYAGO CHA NGURUWE NA DAMU WAKIPINGA MISHAHARA YA WABUNGE
Miungano ya kijamii ikiongozwa na Bunge la mwananchi,Muhuri
na pawa 254 miongoni mwa mengine yameandaa maandamano ya pili kupinga
juhudi za wabunge kuhujumu tume ya kuratibu mishahara nchini kenya SRC
ili kujiongezea mishahara ya hadi laki nane kinyume na ilivyopendekezwa
na SRC.
Tofauti na wiki kadhaa zilizo pita ambapo waandamanaji
waliwaelekeza nguruwe walioandikwa majina ya wabunge walio unga mkono
mswada huo, hii leo waandamanaji walibeba kinyago wa nguruwe na damu
walio ashiria mwisho wawabunge kukandamiza wakenya. huku wakijimwagilia
damu kama ishara ya kuumizwa na kodi ya kuwalipa wabunge.
Waandamanaji pia walibeba mfano wa noti za shillingi alfu
moja pesa za kenya zilizo chorwa Nguruwe mkubwa kwa upande mmoja na
wanawe kwa upande wa pili, huku wakiwarushia wabunge noti hizo kuashiria
kujitakia makuu kwa wabunge hao.
Viongozi wa waandamanaji wameahidi kuendeleza maandamano hadi
pale wabunge watakapo sitisha hujuma dhidi ya tume ya bi sara serem ama
SRC.
Tume ya SRC imependekeza wabunge kulipwa mshahara wa kati ya
shillingi laki Nne hadi laki saba.Ilihali wabunge walipendekeza mshahara wa
hadi shillingi millioni moja.
Wa k nooma
ReplyDelete