Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye mitandao mbalimbali nchini Tanzania, mrembo huyu, mwanamuziki Feza Kessy, ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika Big Brother Africa 2013 (BBA “The Chase.” Well, hizi ni baadhi ya picha zake. Tunaenda vizuri, bahati inaonekana kutuangukia watanzania kwani mshiriki Feza jana ameukwaa ukuu wa kaya ama kwa lugha ya ki-big brother ‘Head of House’. Ilikuwaje? Baba mwenye nyumba, biggie, alitoa task ambayo washiriki walitakiwa kuelekea bustanini na kuchagua box, ambaye angechukua box la ushindi ndo huyo angekuwa mkuu wa kaya. Kama zali, bahati hiyo ilimuangika mrembo Feza. Washiriki wenzie akiwemo mtanzania Nando, walimkumbatia kwa furaha kama ishara ya kumpongeza. Iko hivi, ukichaguliwa kuwa mkuu wa kaya, unauwezo wa kumuokoa mtu ambaye anakuwa amependekezwa atoke katika wiki hiyo. Usipofanya hivyo basi wewe mwenyewe unawekwa kikaangoni. Feza alitumia nafasi hiyo kumuokoa Elikem ambaye ni mshiriki k...