P- FUNK AWACHANA TENA CLOUDS FM....
AELEZA JINSI MAREHEMU NGWEA ALIVYOGEUZWA NG'OMBE WA MAZIWA
Kwa mara nyingine tena P-Funk amezungumzia sababu anazodhani zilipelekea marehemu Ngwea kujiingiza kwenye madawa.
Producer huyo ameichana CloudsFM kwa kile anachokiona kama unyanyasaji kwa wasanii, na kwamba dhuluma za Clouds Fm ni moja wapo ya vitu vilivyosababisha maisha ya Ngwear yawe na muelekeo mbaya.
“Ngwair alikua kama ng’ombe wenu; mnamkamua tu maziwa.” P funk
Akizungumzia kuhusu kuikataza Clouds FM kupiga nyimbo za Bongo Records zikiwemo wa Ngwea, P-Funk amesema:
“Niko
kwenye harakati za kuandaa barua ili nistopishe nyimbo zangu zote za
Bongo Records, zisipigwe Clouds Fm.
Sababu
kubwa ni uonevu wa haki miliki. Eti mnajiita number one radio
station??. Mnajidaganya .Kisaikolojia wasanii wote mmewateka.
Wote
wanaona “bila kupeleka nyimbo zao Clouds hawatafanikiwa.” Mimi cha
kwanza nataka kuonyesha mfumo mwingie kwamba bila nyinyi tutaweza. Cha
pili mnaingiza hela sana ya wadhamini lakini hamui-distribute kwa
wanaohusika...
"Mfumo wa
kupeleka nyimbo Clouds nilianzisha mimi . Hivyo nitakua wa
kwanza kujitoa na kuanzisha mfumo mwingine.””
Comments
Post a Comment