SIMBA YASEMA KUONDOKA KWA NGASA HASUMBUI
Simba:Ngasa hatusumbui kichwa
Kwa ufupi
- Mwanzoni mwa wiki hii, Ngassa alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, klabu aliyoichezea kabla ya kujiunga na Azam FC na kisha kutua Simba alikocheza msimu mmoja uliomalizika wiki iliyopita
Baada ya
siku mbili tu kupita tangu winga wa Simba, Mrisho Ngasa ajiunge Yanga,
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage amesema kuondoka kwa mchezaji
huyo hakuwasumbui hata kidogo.
Mwanzoni mwa wiki hii, Ngassa alisaini mkataba wa
miaka miwili kuichezea Yanga, klabu aliyoichezea kabla ya kujiunga na
Azam FC na kisha kutua Simba alikocheza msimu mmoja uliomalizika wiki
iliyopita.
Simba wanadai Ngassa alikuwa tayari amesaini
mkataba wa miaka miwili kwao, kabla ya kusaidi wa Yanga jambo linalizua
utata kwenye klabu hizo mbili kongwe nchini.
Akizungumza kwa simu jana, Rage alisema haipo
sababu ya kuumiza vichwa kuhusu Ngassa kwani sheria za usajili ziko wazi
na kufahamika kwa kila mtu.
“Sheria ziko wazi, hatuna sababu za kuumiza
kichwa. Kwa sasa tunajipanga kufanya usajili siyo tena kufuatilia mambo
ya Ngassa,” alisema Rage.
“Hatuwezi kila siku kukaa na kuzozana kuhusu
sheria...Ngassa hawezi kutuumiza kichwa, tuna mambo mengi ya kufanya
ikiwa kujipanga kwa ajili ya usajili.
“Sheria ziko wazi na mkataba wake na sisi upo TFF, hivyo muda utakapofika kila kitu kitawekwa wazi,” alisema Rage kwa kujiamini.
Aidha, Khalfan Ngasa ambaye ni baba mzazi wa
mshambuliaji Ngassa amewataka mashabiki wa soka hususan wale wa Simba
wasimchukie mwanae kutokana na uamuzi wake wa kurejea Yanga.
Akizungumza na Mwananchi, Khalfan alisema kuwa
uamuzo kuhama timu moja na kujiunga na nyingine ni kitu cha kawaida,
hivyo mashabiki Simba wasichukulie kama ni usaliti.
“Nadhani tuheshimu uamuzi wake kwasababu katika
soka hilo ni jambo la kawaida kuhama timu moja na kwenda nyingine na
ndiyo maana alitoa Yanga, akaenda Azam, Simba na sasa ameamua kurudi
Yanga.
“Yule ni mtu mzima hata mimi siwezi kumpangia
mambo yake, sana sana kama baba yake kazi yangu ni kuhakikisha anapata
haki zake kama kawaida,”. alisema Ngassa ambaye ni kocha wa timu ya
Polisi Iringa.
Katika hatua nyingine uongozi wa Simba umesema
umepangwa kutumia kiasi cha dola za Sh40 milioni katika ujenzi wa uwanja
wao ulipo Boko nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Comments
Post a Comment