WANAWAKE WA DODOMA WAJITOKEZA KWA WINGI KUCHANGAMKIA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA MANJANO FOUNDATION
Wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanaonufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers wakikisikiliza kwa Makini Mada Kuhusu Elimu ya Biashara na namna ya kuendesha Ujasiriamali Kwenye Mafunzo Yanayoendelea Mkoani Dodoma . Mafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano yameanza mkoani Dododma. Jumla ya Washiriki 30 wamechaguliwa katika fursa hiyo na wanajulikana kama Manjano Dream Makers. Mafunzo hayo yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza wanawake hao kutoka Manispaa ya Dodoma watapatiwa elimu kuhusu sifa za ujasiriamali, changamoto zake na namna ya kukuza na kuendesha biashara ikiwa pamoja na nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani 'Financial literacy'. Pia washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja na kujua mbinu zipi watumie kujiwekea akiba. Afisa Mtendaji Mkuu wa Shera Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Akieleza Machache leo wakati wa Mafunzo y