Linah afunguka kuhusu unene wake.

Mwanadada Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa swala la kuongezeka kwa mwili wake baada ya yeye kujifungua hakuathiri kazi zake kwa sababu anaweza kufanya kitu chochote jukwaani kuwafurahisha mashabiki wake,


Hii inakuja baada ya moja ya picha yake ya wikiendi hii kusambaaa sana katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa kama amenenepa sana na kuwa anaweza kushindwa kufanya show nzuri kama zamani,

Akiongea na  Clouds fm Linah anasema; "Mazoezi nafanya ya kawaida tu, naupenda sana mwili wangu, mimi naona kawaida tu kuongezeka kwangu hakujaniathiri chochote nafanya kazi zangu kama kawaida, napiga shoo jukwaani na najiona ni mwepesi kama kawaida, unajua kuwa watu wembaba lakini wazito, lakini mimi unene nilionao haunipi changamoto zozote ninapokuwa jukwaani nawaburudisha mashabiki wangu kama kawaida, halafu ujue kwamba mimi sio dansa mimi ni mwanamuziki naimba nitakavyo sio lazima niruke ruke"

Comments

Popular posts from this blog