Zari Awapiga Stop Wema, Aunt: Sitaki Kunichafulia Nyumba, Kaeni Hukohuko

IKIWA ni saa chache baada ya mwanamuziki Diamond Platnumz kualika watu takribani 50 kuuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mtoto wake  Tiffah, mzazi mwenzake, Zari Hassan amepiga marufuku ugeni huo.
Jana wakati wa sherehe ya kufikisha siku 40 ya mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema, Diamond alialika wanakamati zaidi ya 10 kuhudhuria sherehe hiyo ya Tiffah, Sauzi hukuakisema atalipia tiketi za watu 30 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe na kuwalipia watoto 10 na wazazi wao.
Hata hivyo, Zari amemjibu kupitia mtandao wa Instagram aliandika kuwa hautaki ugeni huo akihofia kuchafuliwa nyumba yake: “Sitaki kunichafulia nyumba kaeni hukohuko.”
Miongoni mwa wanakamati walioalikwa ni Wema Sepetu ambaye amewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz na mwigizaji Aunty Ezekiel. Tiffah ambaye jina lake halisi Latiffah alizaliwa Agosti 6, 2015. Hata hivyo sherehe za kuzaliwa binti huyo zitafanyika siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 17- 19 mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog