FT: Simba 2-1 Stand United Uwanja wa Taifa, Dar



Wachezaji wa timu ya Simba wakipongezana.
FT: Mpira umemalizika na Simba wanaibuka na ushindi wa bao 2-1
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.
Dakika ya 87: Kasi ya mchezo imepungua.
Dakika ya 83: Rajab Rashid anaingia kuchukua nafasi ya Aaron Lulambo Upande wa Stand.
Dakika ya 80: Simba wanafanya shambulizi kali lakini mabeki wa Stand wanakuwa makini kuokoa
Dakika ya 79: Abdi Banda wa Simba anaingia kuchukua nafasi ya Kichuya.
Dakika ya 78: Simba wanaonekana kupoteza umakini katika nafasi wanazopata.
Dakika ya 74: Mavugo anaachia mkwaju mkali, unamtoka kipa lakini anawahi kuudaka tena.
Dakika ya 66: Kichuya anapata nafasi langoni mwa Stand lakini anashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 66: Kichuya anapata nafasi langoni mwa Stand lakini anashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 65: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Luizio, anaingia Pastory Athanas.
Dakika ya 61: Stand wanafanya shambulizi kali, kipa wa Simba anafanya kazi nzuri inakuwa kona.
Dakika ya 60: Straika wa Simba, Juma Luizio anakuwa msumbufu kwa walinzi wa Standa mara kadhaa.
Dakika ya 57: Job anatoka nje kupatia matibabu, baada ya muda anarejea uwanjani.
Dakika ya 55: Beki wa Stand, Ibra Job yupo chini ameumia, mwamuzi anaita madaktari wanaingia kumtibu.
Dakika ya 51: Simba wanapata kona lakini wanapiga kona fupi na haizai matunda.
Dakika ya 50: Simba wanafanya mabadiliko, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Mwinyi Kazimoto.
Dakika ya 49: Beki wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ anachezewa faulo na mpira unapigwa kuelekea kwa Stand.
Mwamuzi anapuliza filimbi kuanza kwa kipindi cha pili.
Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.
MAPUMZIKO
Dakika ya 49: Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza kipindi cha kwanza. Simba inaongoza kwa mabao 2-1.
Dakika ya 45: Zimeongezwa dakika 4 za nyongeza.
Dakika: 44: Laudit Mavugo wa Simba anashindwa kutumia nafasi anayopata akibaki yeye na kipa, kipa wa Stand anauwahi mpira miguu kwake.
Dakika ya 42: Simba wanaonyesha kuwa na nguvu ya kuendelea kushambulia.
Dakika ya 37: Frank Hamis wa Stand United anapata kadi ya njano kwa kumzonga mwamuzi akipinga bao.
Dakika ya 35: Simba wanapata bao la pili baada ya mabeki wa Stand kudhani ameotea, mfungaji ni yuleyule wa bao la kwanza Juma Luizio, wachezaji wa Stand wanaendelea kuzungumza na mwamuzi wa kati wakilalamika kuwa mfungaji aliotea.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!
Dakika ya 32: Simba wanazidisha mashambulizi, lakini mara kadhaa wachezaji wa Stand wanazungumza na mwamuzi wa kati wakionekana kulalamika.
Dakika ya 26: Mashabiki wa Simba sasa wameamka na wanashangilia toafauti na ilivyokuwa awali, Simba wanalishambulia lango la Stand.
Dakika ya 23: Simba wanapata bao la kusawazisha kupitia kwa Juma Luizio
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 23:  Simba wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 19: Simba wanarudisha mpira nyuma na kuanza kujipanga kutokea nyuma.
Dakika ya 15: Mchezo unaanza kushika kasi, timu zote zinamiliki mpira hasa katikati ya uwanja.
Dakika ya 10: Simba wanamiliki mpira muda mwingi lakini Stand nao wanawadhibiti na kujipanga vizuri.
Dakika ya 5: Bado Simba wanaonekana kujaribu kutulia.
Dakika ya 2: Simba wanaanza kujipanga taratibu
Mfungaji wa bao hilo ni kiungo mshambuliaji wa Stand United, Kassim Selembe
Stand United wamepata bao katika sekunde za mwanzoni tu za mchezo huu baada ya kipa na beki wake kufanya uzembe.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!
Mchezo ndiyo kwanza umeanza,
Mchezo huu wa Simba dhidi ya Stand United utachezwa hapa kwenye Uwanja wa Taifa ni wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Kikosi cha Simba kitakachoanza ni:
1-Daniel Agyei
2-Javier Bukungu
3-Mohamed Hussein
4-James Kotei
5-Juuko Murshid
6-Jonas Mkude
7-Shiza Kichuya
8-Mzamiru Yassin
9-Laudit Mavugo
10-Juma Luizio
11-Mohamed Ibrahim
SUB
-Peter Manyika Jr
-Vincent Costa
-Novart Lufunga
-Abdi Banda
-Mwinyi Kazimoto
-Pastory Athanas
-Fredrick Blagnon

Comments

Popular posts from this blog