WAZIRI MAHIGA AONGOZA TIMU YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC UCHAGUZI WA JAMHURI YA SHELISHELI
Waziri
wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustino
Mahiga akifungua Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge
tarehe 2 Septemba, 2016, Mahe Seychelles. Mhe Waziri anamuawakilisha
Mhe. Rais John pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya
SADC.
Waziri
wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya
pamoja na Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2
Septemba, 2016 huko Mahe, Seychelles.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine
P. Mahiga (Mb.), jana tarehe 2 Septemba, amezindua Misheni ya Waangalizi
wa Uchaguzi wa SADC kwenye uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli kwa niaba
ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya
ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika -SADC Organ.
Misheni
hiyo ya waangalizi wa uchaguzi itakayojumuisha waangalizi kutoka nchi
za SADC, itashiriki kwenye uangalizi katika vituo vyote 25 vya upigaji
kura nchini Shelisheli.
Pamoja
na kuongoza misheni hiyo, Tanzania kama Mwenyekiti wa SADC Organ
itaongoza timu za uandishi wa taarifa ya SADC pamoja na ufuatiliaji wa
taarifa za vyombo vya habari kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi nchini
humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 8-10 Septemba, 2016.
Tanzania
ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza asasi hii muhimu ya
Jumuiya, wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali
uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016.
Mara
baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mhe. Dkt. Mahiga, Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya
Shelisheli kumwakilisha Mhe. Dkt. Magufuli, katika kuongoza ujumbe wa
Waangalizi wa SADC.
Wajibu
wa Tanzania kuongoza Misheni hya Waangalizi wa Uchaguzi imetokana na
misingi na muongozo wa Jumuiya ya SADC ya kuwa na chaguzi za
kidemokrasia katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ya Maendeleo ya
Kusini mwa Afrika. Waziri Mahiga anatarajiwa kutoa taarifa ya awali ya
Misheni hiyo ya waangalizi wa SADC Septemba 12, 2016.
Comments
Post a Comment