UHURU KENYATTA AKANUSHA KUWEPO MVUTANO WA KIUCHUMI KATI YA TANZANIA NA KENYA
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumamosi alikanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba kuna mvutano baina ya Kenya na Tanzania.
Akizungumza
mjini Mombasa wakati wa ufunguzi gati la makontena katika bandari ya
Mombasa, Kenyatta alipuuzia maneno kwamba kuna mvutano wowote na badala
yake akasema kuwa nchi hizo zinasaidiana.
Alisema
anaona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna “mgogoro baina yetu, lakini
nataka kusema wazi wazi kwamba Kenya na Tanzania hazina mgogoro wowote
baina yao,” alisema.Kenyatta alisema uchumi wa nchi hizo mbili
umefungana kwa miaka mingi na ni kwa ajili ya faida ya watu wa nchi hizo
mbili.
Alitaja
kufunguliwa kwa njia inayojulikana kama “northern frontier” ambayo
itaunganisha bandari ya Mombasa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania,
hadi Bujumbura, Burundi – njia ambayo itafupisha urefu wa kutoka
Bujumbura hadi Mombasa kwa kilomita 300 nzima.
“Afrika
Mashariki haiko katika mashindano ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema
Kenyatta. “Afrika Mashariki inashindana na dunia. Tunataka kujaliana
(pale penye mapungufu). Tunataka tutumie nguvu zetu ili kukua,
kuendeleza na kuinua uchumi wetu,” alisema.
Kutokuwepo
kwa Rais John Magufuli wa Tanzania katika mkutano wa hivi karibuni wa
kimataifa na Tokyo mjini Nairobi kulizusha uvumi kuhusu uhusiano wa nchi
za eneo hilo.
Kiongozi
huyo wa Tanzania ametembelea Uganda na Rwanda tu tangu achukue madaraka
Oktoba mwaka jana ukilinganisha na rais aliyemtangulia Jakaya Kikwete
ambaye alikuwa akisafiri sana nchi za nje.
Rais
Magufuli pia hakuhudhuria mikutano karibu mitano ya kimataifa, ikiwa ni
pamoja na mkutano wa shirika la biashara duniani na mikutano mikuu ya
AU mjini Addis Ababa na ule wa Kigali Rwanda hivi karibun
Comments
Post a Comment