Polisi Wafyatua Risasi & Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa Lipumba
Jeshi
la Polisi limelazimika kufyatua risasi angani na kutumia mabomu ya
machozi kuwatawanya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaodhaniwa
kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba
waliokuwa wakimzuia mwenyekiti wa muda wa CUF, Julius Mtatiro, kuingia
ofisini eneo la Buguruni.
Wafuasi hao wameeleza kuwa wameamua
kumzuia kwani Msajili wa Vyama vya Siasa ametaka shughuli zozote ndani
ya CUF zisiendelee hadi hapo mgogoro wa uongozi utakapotatuliwa.
Itakumbukwa hivi karibuni CUF
kilimteua Julius Sunday Mtatiro kuwa mwenyekiti wa muda baada ya
mwenyekiti aliyekuwepo, Prof. Lipumba kijiuzulu Agosti 2015.
Julius Mtatiro leo amefanya mkutano na
waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar
es Salaam ili kuzungumzia kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa visiwani Zanzibar.
Comments
Post a Comment