Posts

Wasiotumia EFDs Marufuku Kufanya Biashara na Serikali

Image
KUANZIA Julai mosi mwaka huu, serikali imepiga marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema hayo jana bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma jana. Aidha, Dk Mpango aliwapongeza wafanyabiashara walioitikia matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ambayo inamtaka kila mfanyabiashara isipokuwa wale ambao wametangazwa rasmi na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato kutotumia mashine za EFD kutoa risiti kila anapouza bidhaa au huduma. Alisema ili kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuhakikisha kwamba zinatumika kama ilivyokusudiwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Fedha za Umma na kanuni zake, alitangaza kuwa malipo yote lazima yaambatanishwe na ankara za madai au stakabadhi (tax invoice) zilizotolewa na mashin

Huu Hapa Mchanganuo wa Bajeti ya Serikali 2016/ 2017

Image
SERIKALI imewasilisha Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 ya Sh trilioni 29.53, ambayo nguvu kubwa imewekwa katika kukusanya mapato kwa kulinda viwanda vya ndani na kubana matumizi ya serikali ili kuelekeza sehemu kubwa ya matumizi katika maeneo ya vipaumbele. Katika bajeti hiyo, bidhaa za lazima zinazogusa maisha ya wananchi ikiwemo mafuta ya petroli na dizeli pamoja na ushuru wa barabara na maji ya kunywa, havijaguswa huku bidhaa za starehe kama bia, sigara, soda, juisi na nyingine kama nguo za mitumba, huduma za kupanga nyumba na uhamishaji fedha kwa simu, vikipandishwa kodi, huku kiinua mgongo cha wabunge, kufutiwa msamaha wa kodi. Aidha, makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi, ikiwemo mapato ya taasisi za udhibiti kama Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Mafuta (EWURA), Shirika la Viwango (TBS), Jeshi la Polisi (Trafiki) na mamlaka nyingine za udhibiti, sasa yatapelekwa moja kwa moja katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo mahitaji yao ya fedha yatatolewa na Wizara ya

KARIBU UJUMUIKE NA WAZAZI WENZAKO KWENYE JUKWA LA KUJADILI MALEZI YENYE MALENGO

Image
Ni ukweli usiopingika kuwa waazazi wote hupenda kuona watoto wao wakikua katika maadaili yanayopendeza na ikiwemo kufaulu vizuri katika masomo yao na hata wafikiapo umri wa kujitegemea wawe vijana wenye maono bora. Hapo nyuma hakukuwa na mitaala ya kuweza kuwasaidia wazazi kukuza watoto vile inavyotakikana, hivyo ilipelekea watoto wengi kushindwa kufikia malengo yao na lawama walitupiwa wazazi wao. Njoo ujiunge sasa na wazazi wenzako kwa mara ya kwanza Tanzania inakuletea (Malezi yenye malengo) ni jukwaa la majadiliano,maoni,na njia mbadala za kuwalea watoto wetu. Nafasi ni chache jisajili mapema Karibuni sana. Wazungumzaji watakuwa Mrs Grace Makani Tarimo kutoka  Grace Inc Ltd na Dr. Elie Waminian (PHD) Kutoka Marekani Namba ya simu 0754-46174 11/06/2016. Hyatt Regency Hotel

TIMU YA ENGLAND YAWASILI PARIS UFARANSA KWAJILI YA EURO

Image
Kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya England kimewasili Paris Ufaransa mchana wa leo June 6 2016 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016, England imeondoka Lutonasubuhi na kuwasili Paris Airport-Le Bourget mchana wa leo June 6 2016, Englanditacheza mchezo wake wa ufunguzi wa Euro 2016 Jumamosi hidi ya Urusi.

RAIS DKT MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA RAIS WA SAHARAWI, AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA UBELGIJI, BALOZI WA MAREKANI NA KUAGANA NA BALOZI WA ITALY

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italy nchini Mhe. Luigi Scotto  aliyemtembelea na kumuaga baada ya kumaliza muda wale wa kazi Ikulu Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italy nchini Mhe. Luigi Scotto  aliyemtembelea na kumuaga baada ya kumaliza muda wale wa kazi Ikulu Dar es salaam leo. Rais

TAARIFA YA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKALA WA UAGIZAJI WA MAFUTA KWA PAMOJA (PBPA)

Image
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb), amemteua Dk. Steve Mdachikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kuanzia tarehe 03 Juni, 2016. Kufuatia uteuzi huo, amewateua pia wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PBPA kuanzia tarehe 03 Juni, 2016. 1. Dkt. Daniel Sabai 2. Dkt. Henry Chalu 3. Dkt. Siasa Mzenzi 4. Mr. Salum Mnuna Imetolewa na; KATIBU MKUU 6 Juni, 2016

TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA KODI KWA MWEZI MEI 2016

Image
MKamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata akitilia mkazo jambo wakati wa kikao na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwezi Mei 2016,kilichofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abdul Mapembe. MAMLAKA ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.032 katika mwezi Mei ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.025 katika mwezi huo. Makusanyo ya kipindi cha miezi kumi na moja (Julai 2015 hadi Mei 2016) ni jumla ya shilingi trilioni 11.956 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la shilingi trilioni 12.054 katika lengo la kipindi hicho kwa Tanzania Bara na Zanzibar. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata amesema TRA inaendelea na jitihada mbalimbali kuhakiki

MSANII DIAMOND ATOA MSAADA WA MADAWATI 600 KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE. MAKONDA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Mkoa wetu. Akiongea katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika kukabilana na changamoto za elimu. Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake k

Polisi Jijini Mwanza Wapambana na Majambazi kwa Saa 16, Wakamata Silaha Nzito, Watatu Wauawa

Image
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkia jana jumapili katika mapango ya mlima wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini Mwanza. Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,amewataja majambazi waliouwa katika majibizano ya risasi usiku kucha kuwa ni Omar Francis Kitaleti mkazi wa Nyegezi Kona,said Khamis Mbuli maarufu kama fundi bomba mkazi wa bugarika na jambazi mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika. Amesema majambazi hayo yalikuwa yamejificha kwenye mapango ya mlima wa Utemini kabla ya askari polisi kufanikiwa kuyaua. Jambazi mmoja aliyeuawa ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 25 alikuwa akiwashambulia polisi kwa kutumia bastola ambapo baada ya polisi kumpiga risasi walimpekua na kumkuta akiwa na bastola aina ya Chinese,iliyokuwa na risasi tatu ndani ya magazine,huku majambazi wengine waliokuwepo kwenye mapango hayo wakiendelea kujibishana kwa

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA IBADA KATIKA KANISA LA MAOMBEZI LA MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO UBUNGO KIBANGU LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabarainayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo‘mzee wa upako akiagana na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada yakuhudhuria ibada katika Kanisa la Maombezi Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru waumini wa kanisa hilo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa la Maombezi la Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)

11 Certain Signs He’s Ready For A Serious Relationship

Image
The beginning of a relationship can be a cloudy thing – it’s hard to determine if someone is just playing you and feeding you words you want to hear, or if they’re sincere and really care about you. Here’s a guide to weeding out the bad guys from the good ones, and seeing who’s willing to go past the casual phase and dive into something real. 1. He’s stopped seeing other people and wants to be exclusive. He wants to see you on Friday and Saturday. He’s so into you, he can’t even think about other girls, because you’re the only one that really makes him happy. He knows building a real foundation with you means getting serious with exclusivity, and he’s into it. 2. He’s starting using the we word. That means he visualizes himself with you, and wants to get serious with you. He wants to make more memories with you, and wouldn’t use that word if he couldn’t see himself with you.  3. He’s open about his insecurities with you. He talks about his struggles, with confidence and

Hawa Wamechinjwa Bila Hatia!

Image
Marehemu Mkiwa Philipo. Stori: Oscar Ndauka,  Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM  na mikoani: Inauma sana! Ndilo neno ambalo linafaa kutumika kwa sasa kufuatia kuibuka kwa mauaji  kwa njia ya kuchinja sehemu mbalimbali za nchi hali inayoibua hofu kwa wananchi,  Risasi Jumamosi  limechimba na kuibuka na ripoti kamili. TUKIO JIPYA Tukio bichi kabisa ni lile la Mei 31, mwaka huu kwenye Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Manispaa ya Tanga ambapo watu 8 wameuawa kwa kuchinjwa shingo kikatili na watu wasiojulikana, madai yakitajwa kuwa ni kisasi. Marehemu Eugenia Philipo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul, aliwataja watu hao kuwa ni Mjumbe wa Serikali ya Kijiji, Issa Hussein (50), Mkola Hussein (40), Hamisi Issa (20) na Mikidadi Hassan (70). Marehemu Anathe Msuya Wengine ni Mahmoud (anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 hadi 40), Issa Ramadhani (25) na wachunga ng’ombe wawili walilofahamika kwa jina mojamoja, Kadiri na Salum. Kwa hesabu za jumla, mpa

ZARI THE BOSS LADY NI MJAMIZITO TENA.MAMA YAKE DIAMOND ATHIBITISHA KWA MANENO HAYA

Image
Muda si mrefu sana toka Zari na Diamond Platnumz wamepata mtoto wao wa kwanza kwa jina Kupitia mtandao wa Instagram Mama wa Diamond Platnumz amepost picha ya pamoja akiwa na Diamond Platnumzpamoja na Zari na kuandika "ETI MAMA .K...".

JACQULINE MENGI ATIKISA MITANDAO YA BONGO LEO LIVE

Image
Posted these many faces of hers while rocking the bob hair style with a bright red lipstick on Ready for a business meeting?? The mother of two wore a blush of pink skirt and a bow top with nude shoes,

MAUZAUZA NYUMBANI KWA WAZIRI WA MAGUFULI,JIONEE HAPA

Image
Bibi kizee alivyonaswa usiku akirandaranda na tunguri nyumbani kwa Waziri Mwigulu Nchemba. DODOMA:  Katika hali isiyo ya kawaida bibi kikongwe mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake, amezua sintofahamu baada ya kukutwa nyumbani kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akizunguka nyumba yake usiku huku akiwa na tunguri na wembe wenye damu. Tukio hilo lilitokea Mei 31, mwaka huu majira ya saa 6 usiku katika eneo la Kilimani mjini Dodoma kwenye nyumba ya waziri huyo ambako ni makazi ya mawaziri na viongozi mbalimbali wa umma. Akizungumza na mwandishi wetu, eneo la tukio, shuhuda wa tukio hilo, Sumai Juma alisema kuwa alimwona mwanamke huyo  akiwa amekumbatia vitu vyake akizunguka nyumba ya waziri. Baada ya kumwona mtu huyo, alilazimika  kuita mlinzi na kujaribu kumhoji bila mafanikio kutokana na mwanamke huyo kutojua lugha yoyote na kila anachoulizwa alikuwa hajibu zaidi ya kurudia maneno yaleyale ambayo alikuwa akimuulizwa. “Huyu kikongwe alikuwa kama na