Mwili wa Papa Wemba Wawasili DRC
Kinshasa, Kongo
Mamia
ya watu wamekusanyika leo nje ya Uwanja wa Ndege wa Kinshasa nchini
Kongo wakisubiri mwili wa mwanamuziki aliyefariki Jumapili iliyopita,
Papa Wemba kuwasili nchini humo.
Maafisa wa serikali na wanadiplomasia
watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege
kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba.
Mwanahabari wa BBC Tamasin Ford anasema
kuwa mashabiki wengi walivalia nguo nyeusi na kubeba mishumaa ili kutoa
heshima kwa nguli huyo wa muziki.
Mkewe Papa Wemba na wasaidizi wake pia walikuwepo.
Papa Wemba, who died aged 66, was considered one of Africa’s most influential musicians of his generation.He pioneered modern Congolese soukous music, which spread through the continent.
Comments
Post a Comment