Posts

DAVID DE GEA AWEKA REKODI USIKU WA TUZO MAN UNITED

Image
David De Gea ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Manchester United kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Jumatatu usiku kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo. De Gea ametwaa tuzo hiyo maarufu kama Matt Busby player of the year ikiwa ni baada ya kutoruhusu kufungwa bao lolote katika michezo 14 kati ya 32 ya Ligi Kuu England aliyoicheza Manchester United msimu huu wa 2015/2016 huku pia akifanya vizuri katika michuano ya kombe la FA.Mbali ya De Gea nyota mwingine aliyewahi kutwaa tuzo hiyo kubwa zaidi mara tatu lakini katika vipindi tofauti ni Mreno Cristiano Ronaldo. Ronaldo alitwaa tuzo hiyo mwaka 2004, 2007 na 2008. Akiongea baada ya kutwaa tuzo hiyo De Gea amesema: “Ni ngumu kusema chochote, kutwaa tuzo hii mara tatu mfululizo ni faraja na heshima kubwa. Napenda kuwashukuru mashabiki wetu ambao ni bora zaidi duniani”. Wengine walioshinda tuzo Jumatatu usiku ni: Chris Smalling aliyetwaa tuzo ya mchezaji

NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015

Image
Kamati Maalum iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume. Akizungumza Katika kikao cha Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa niaba ya Wajumbe wa Tume amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa. Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume imeridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ikiwa ni pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo. Aidha, ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema mwezi Julai mwaka huu. Pongezi hizo pia zimetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchagu

NAFASI ZA KAZI MWANANCHI MWISHO WA KUTUMA MAOMBI TAREHE 13 MAY 2016

Image
FREELANCER BUSINESS EXECUTIVE-TANGA POSITION DESCRIPTION: Mwananchi Communications Limited publishers of leading Tanzania newspapers, Mwananchi, Mwanaspoti and The Citizen are looking for motivated and highly experienced individuals to fill the positions of: – Freelancer Business Executives (16 POSTS) Dar es Salaam (8), Mtwara (1), Lindi (1), Dodoma (1), Singida (1), Zanzibar (1), Tanga (1), Kigoma(1) and Tabor(1). Job Purpose: To develop, maintain and increase a solidly dependable client base, to sell advertising space and provide an effective service to clients so as to maximise advertising sales volumes and revenue targets. . Main Responsibilities: • The successful candidates will be responsible for the following key result areas: • Thoroughly familiarizes oneself with comparative (own and competition) readership, circulation and rates and cost of advertising in all print and electronic media. • Identifies potential advertising clients, studies their bus

Aliyejifungua Watoto 3 Aomba msaada

Image
MKAZI wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Julietha Sokoine (24) amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali, taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha utakaomsaidia kuwatunza watoto hao. Pia alisema msaada huo pia utamuwezesha kupata tiba ya ugonjwa wa pumu ambao umemsababisha kuvimba mwili wote. Akizungumza mwishoni mwa wiki, Sokoine ameiomba jamii kumsaidia kutokana na kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu ambao pia umesababisha kuwa na hali ngumu ya kimaisha ambayo inamfanya kushindwa kuwatunza vizuri watoto wake. Alisema watoto hao, Daniel Sokoine,David Sokoine na Davis Sokoine walizaliwa kwa pamoja Machi 22, mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Dodoma huku kati ya wawili wa wakiwa na uzito kilo mbili na nusu na wa mwisho kilo mbili. “Hali yangu siyo mzuri kutokana na mimi mwenyewe kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu,ambapo wakati mwingine nalazimika kuwanywesha maziwa ya ngombe watoto hao

Maelfu wamuaga Papa Wemba Kinshasa

Image
 Papa Wemba atazikwa Jumatano Maelfu ya waombolezaji walijitokeza kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota wa muziki wa Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo Papa Wemba. Waomboloezaji walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma lililopita alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko Abidjan Ivory Coast. Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi kuanzia leo hadi jumatano atakapozikwa. Tayari amepewa tuzo kwa mchango wake. Maelfu watarajiwa kujitokeza kumuaga Papa Wemba Faly Ipupa na mashabiki waulaki mwili wa Papa Wemba Historia ya Papa Wemba Msanii huyo nguli alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa Soukus nchini DRC na kote duniani kwa kipaji chake cha kipekee na sauti isiyokuwa na mfano. Wengi waliitambua sauti hiyo ya na utunzi wake. Alikuwa ni mtumbuizaji kamili.  Gwiji huyo wa muziki wa Lingala aliz

MKUU WA CHUO CHA UHASIBU AFUNGWA KWA KOSA LA KUAJIRI WATUMISHI WENYE ELIMU YA DARASA LA 7

Image
MKUU wa Chuo cha Uhasibu (IAA) Njiro mkoani Arusha, Profesa Johannes Monyo amehukumiwa kifungo cha nje kwa sharti la kutofanya kosa lolote ndani ya mwaka mmoja. Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Msofe baada ya kujiridhisha kuwa Profesa Monyo alifanya makosa ya kuajiri watumishi wanane wenye elimu ya darasa la saba bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma. Hakimu Msofe alisema Profesa Monyo akiwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro, aliwaingiza watumishi wanane kwenye ajira ya kudumu bila ya kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Mkuu Utumishi. Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani kwa mashahidi 10 pamoja na vielelezo vinane vilivyotolewa mahakamani hapo na upande wa mshtakiwa kuwa na mashahidi wawili, mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kuwa Profesa Monyo alifanya kosa hilo la kuajiri wafanyakazi hao wanane bila kufuata taratibu za kisheria. “Mahakama imejiridhisha pasip

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANITAREHE 3/5/2016

Image
     

Watahiniwa 75,000 Waanza Mtihani wa Kidato cha Sita Leo

Image
Watahiniwa  74,920 leo wanaanza kufanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Sita katika shule mbalimbali nchini huku watahiniwa 11,597 wakifanya mtihani wa Ualimu. Ofisa Habari wa Baraza la Mitihani (NECTA), John Nchimbi amesema kuwa mtihani wa kidato cha sita unaanza leo hadi Mei 19, mwaka huu. Nchimbi amesema kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 65,610 ni watahiniwa wa Shule huku watahiniwa wa Kujitegemea wakiwa 9,310. “Kati ya watahiniwa wa shule 65, 610, watahiniwa wasichana ni 24,549 na wavulana ni 41,061 huku watahiniwa wa kujitegemea wasichana wakiwa ni 3,176 na wavulana ni 6,134,” alisema Nchimbi. Kwa upande wa mtihani wa ualimu, Nchimbi amesema kati ya watahiniwa 11,597 watakaofanya, watahiniwa 10,942 wanafanya Ualimu Daraja A na watahiniwa 654 wanafanya mtihani wa Stashahada ya Sekondari na mmoja anafanya Stashahada ya Ufundi.   “NECTA inatoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa, na wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zote za mit

Mahakama ya Kisutu Yatoa Hati ya Kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob

Image
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar imetoa hati ya kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob (Pichani)kutokana na kutofika mahakamani. Meya huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia  mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na kumsababishia maumivu makali. Kesi hiyo jana ililetwa mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa ajili ya usikilizwaji ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja. Wakili wa serikali Onolina Mushi alidai kwamba,kesi hiyo ililetwa kusikilizwa lakini mshitakiwa pamoja na wakili wake hawajafika mahakamani. Kutokana na hali hiyo,aliiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na kupanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza shauri hilo. Hakimu alikubali maombi hayo ikiwemo ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa Meya huyo.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji. Katika kesi hiyo,Boniface anadaiwa kutenda kosa hilo  Septemba 11, mwaka jana, maeneo

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016.PICHA NA IKULU.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WAFANYAKAZI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOANI DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kombe la ushindi wa jumla kwa Rais wa TUCTA Gratian Mukoba katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Cheti cha Mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Ndugu Peter Chisun

RAIS MAGUFULI ASHUSHA KODI YA MAPATO YA MSHAHARA (PAYE) KUTOKA ASILIMIA 11 HADI 9

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli  ametangaza kushusha kodi ya mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -PAYE  )  kutoka asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9. Rais amesema ameamua kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuwapunguzia mizigo wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara na kuwapunguzia kodi ya mapato ya mishahara. Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya Rushwa. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa

DK. SHEIN AONGOZA SIKU YA KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI ZANZIBAR

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi,  wakipita mbele yake wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi,(pichani) Vijana waliobeba bango kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili ya Rais akipita mbele yake wakati wa sherehe za sikuya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikul