Neymar afungiwa mechi nne na bonge la faini
Nyota
wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar hatocheza tena michuano ya Copa
America inayoendelea huko Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne
kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokifanya wakati
Brazi ikicheza dhidi ya Colombia mchezo ambao ulimalizika kwa Brazil
kufungwa kwa goli 1-0.
Nahodha
huyo wa Brazil alioneshwa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho ya
mwamuzi kupulizwa kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Santiago
Jumatano iliyopita. Neymar alimpiga na mpira mgongoni kwa makusudi
mchezaji Pablo Armero wa Colombia mara baada ya mwamuzi kupuliza filimbi
ya mwisho kumaliza mchezo huo.
Mshikemshike baada ya Neymar kuzua tafran kwa kupiga mpira ulio ‘mbabua’ mgongoni mchezaji wa Colombia
Awali
alifungiwa kucheza mechi moja, lakini baadae shirikisho la soka la
Amerika ya Kusini (South America Football Confederation) liliongeza
kifungo na faini ya dola 10,000 za Kimarekani baada ya Neymar
kugundulika kuwa alimtolea maneno machafu mwamuzi Enrique Osses raia wa
Chile. Kwahiyo sasa adhabu ya Neymar ni kifungo cha kutocheza mechi nne
pamoja na faini ya dola 10,000 za kimarekani
Naye
Carlos Bacca wa Colombia amefungiwa kucheza mechi mbili na faini ya dola
5,000 za kimarekani baada ya kuhusika kwenye vurugu zilizotokea kwenye
mchezo huo ambapo yeye alimsukuma Neymar mara baada ya kumpiga Armero
kwa mpira.
Lakini
shirikisho hilo la mpira la America ya Kusini limesema, rufaa ikowazi
wa wote waliopewa adhabu na Brazil wanaweza kupinga maamuzi hayo
yaliyotolewa kabla ya mchezo wao wa mwisho wa kundi C dhidi ya Venezuela
utakaopigwa leo (Jumamosi) usiku kuamkia kesho (Jumapili).
Kwasasa
Brazil wanaoongoza kundi C na wanakutana na Venezuela ambao wametoka
kupoteza mchezo wao dhidi ya Peru lakini wakiwa wameshinda mechi yao ya
ufunguzi dhidi ya Colombia.
Awali
Neymar alianza kuonesha vitendo ambavyo si vya kiungwana kwenye soka
pale alipojaribu kufunga goli kwa kutumia mkono lakini baadae
‘akambabua’ na mpira Pablo Armero na kutaka kumpiga kichwa Jeison
Murillo.
Kukosekana
kwa Neymar kutamfanya kocha wa Brazil Carlos Dunga amtumie Robinho kama
mbadala wa Neymar kwenye mechi ijayo dhidi ya Venezuela.
Dunga
amekuwa akiwatumia Robinho na Douglas Costa kwenye mazoezi ili kujaribu
kutengeneza uwiano mzuri kati yao wakati pia kiungo wa Liverpool Philipe
Coutinho anatarajiwa kuanza kwenye mchezo huo ambao utakuwa ni wa
kwanza kwake tangu kuanza kwa mashindano.
Robinho
amejumuishwa kwenye kikosi cha Dunga mwaka jana baada ya kuikosa
michuano ya kombe la dunia wakati huo kocha akiwa Scolari. Robinho
ambaye alishawahi kukipiga Real Madrid, Manchester City na AC Milan
kwasasa anacheza kwenye klabu ya Santos ya Brazil.
Comments
Post a Comment