CHILE YAIUA BOLIVIA 5-0, SANCHEZ KAMA KAWAIDA
Chile
imetoa kipondo cha mbwa mwizi kwa Bolivia baada ya kuichakaza kwa jumla
ya bao 5-0 ikiwa ni mchezo wa kundi A kwenye michuano ya kombe la
Mataifa ya bara la America Kusini almaarufu kama Copa America mchezo
uliomalizika alfajiri ya leo huko nchini Chile.
Charles
Aranguiz alianza kuipatia Chile bao la mapema ikiwa ni dakika ya tatu
tangu mchezo huo kuanza kabla ya winga wa Arsenal Alexis Sanchez kufunga
goli la pili dakika ya 37 na kuifanya Chile iende mapumziko ikiwa mbele
kwa goli 2-0 dhidi ya Bolivia.
Aranguiz
alipachika pao la tatu kwa Chile dakika ya 66 lakini likiwa ni bao lake
la pili kwenye mchezo huo, kabla Gary Medel hajatupia nyavuni goli la
nne dakika ya 80. Zikiwa zimebaki dakika nne ili mwamuzi amalize pambano
hilo, Raldes wa Bolivia alijifunga na kuufanya mchezao huo kumalizika
kwa wenyeji wa mashindano (Chile) kuibuka na ushindi mnono wa goli 5-0.
Aturo
Vidal alikuwepo kwenye kikosi kilichoifanyia mauaji Bolivia akitokea
kwenye sekeseke la ajali ambayo aliipata kutokana na kuendesha gari kwa
spidi kali huku akiwa amelewa. Lakini tofauti na matarajio ya wengi,
Vidal bado alipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa Chile ambao
wamefurahia pia timu yao kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali kwenye
michuanon hiyo.
Miller
Bolanos alianza kuipatia Ecuador bao la kuongoza dakika ya 26 kabla ya
mshambuliaji wa West Ham Enner Valencia kuongeza goli la pili dakika ya
57 kwa upande wa Ecuador. Mexico walipata goli lao la kufutia machozi
dakika ya 64 kwa mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Raul Jimenez.
Comments
Post a Comment