KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AUNGURUMA WILAYANI BUSANDA NA MJI MDOGO WA KATORO MKOANI GEITA LEO.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro, wakati wa ziara Jimbo la Busanda, wilayani Geita, Mkoa wa Geita, ambapo aliwaahidi wachimbaji wadogo wadogo kulitafutia ufumbuzi wa kuwapatia vitalu vya machimbo eneo la Nyarugusu linalomilikiwa na Stamico, wilayani Geita.
Ndugu Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, yupo mkoani Geita kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. eneo la Nyarugusu. 

Comments

Popular posts from this blog