madhara ya sabuni za kurudisha ubikra!!

 
WANAWAKE wameshauriwa
kuacha kutumia sabuni za
kunawia sehemu za siri ambazo
hudaiwa kurejesha ubikira
kwani zina madhara makubwa
ikiwemo kusababisha kansa ya
shingo ya kizazi.
Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi wakati wa uteketezaji dawa,vipodozi na vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.
 
Kazi hiyo ilifanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati. Alisema kumekuwa na sabuni mbalimbali ikiwamo Kaisiki ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira
iliyopotea kurudi kitu ambachosi kweli.


"Sabuni hizo zinapunguza tu
majimaji yaliyo sehemu za siri
za mwanamke jambo ambalo
husababisha wakati wa kufanya
mapenzi mwanaume kupata
ugumu kwenye muingiliano
kwa vile mwili unakuwa
umekataliwa kutoa maji na
hivyo kuleta michubuko kitu
ambacho ni hatari hasa wenye
maambukizi ya magonjwa,"
alisema.
 

Alisema michubuko inapotokea ni rahisi mwanamke kuambukizwa magonjwa ya zinaa hata virusi vya Ukimwi.Mtaalamu huyo alisema sabuni hizo zinatengeneza hali fulani ukeni lakini haiwezi kurejesha
hali ya maumbile iliyopotea. Alisema wanaotumia sabuni hizo wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa na hata kupata saratani ya shingo ya uzazi kwani kemikali zinazotumika katika
kutengeneza sabuni hizo zinaathari kubwa kiafya.

Alisema ni vyema wanawake
wakatambua thamani yao na
kuachana na matumizi ya
sabuni hizo ambazo hazina
manufaa yoyote na badala yake
zimekuwa na madhara
makubwa kwao.

Kwa upande wake, Fredrick Luyangi , Mkaguzi wa dawa kutoka TFDA alisema matumizi ya sabuni hizo huleta athari
kubwa mwilini na wakati mwingine kutengeneza kansa
taratibu bila mhusika kufahamu.

Alisema sabuni hizo
husababisha kansa ya kizazi na
kubainisha sabuni hizo licha ya
kupigwa marufuku zimekuwa
zikiuzwa kwenye maduka ya
vipodozi.

Alisema mara nyingi kwenye
operesheni zinazofanyika
zimekuwa zikiondolewa sokoni
lakini hata hivyo zimekuwa
zikiingizwa kwa wingi hali
inayofanya zoezi la kudhibiti
kuwa gumu.

Alisema ni muhimu kwa
wanawake kuacha matumizi ya
sabuni hizo ambazo zina
madhara makubwa sana kwao
kwani zikikosa wanunuzi
zitaondoka sokoni.


manyandhealthy

Comments

Popular posts from this blog