Faida za kiafya za kunywa maji ya moto

NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO.
Kunywa kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi inaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati.

Wengi wetu huianza asubuhi vyema kwa kikombe safi cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa lengo la kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani. Pale tunakunywa maji, basi wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini kutokana na watalaam wa afya wanavyosema,  tunafanya makosa kufanya hivyo. Mara nyingi unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani majira ya asubuhi, inasaidia kuiponya miili yetu na kuitibu,
kwa kusaidia kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwili ambazo zinaweza kuzuia kinga zetu kuwa katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi.
“matabibu wanasema na kushauri kunywa maji moto ama uvuguvugu nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanyanyo wa maji ya limao, au chai ambayo haina madhara kwa mwili” anasema stella metsovas. Mtaalam katika masuala ya lishe na sayansi ya vyakula alipokuwa akiliambia jarida la Medical Dail.
Utumiaji wa maji moto ama vuguvugu huongeza ukazwaji wa utumbo, ambapo husaidia uondoaji wa vitu visivyotakiwa. Tofauti na maji moto, utumiaji wa maji ya baridi yenyewe huzuia vitu muhimu ikiwemo madini ambayo huwa si rafiki kwa mazingira hayo katika mfumo wa umeng’enywaji unapokula chakula.

Kwa wanywaki wa maji ya baridi, metsovas anashauri kutangulia kunywa maji hayo ya baridi dakika 20 kabla ya kula hata kama maji hayo yanatoka katika vyanzo vya asili vya maji. Wakati unywaji wa maji ya moto ama vuguvugu yanaweza yasiwe mazuri kwa radha yanapokuwa mdomoni,
Hizi hapa zifuatazo ni sababu kwanini unywa maji haya ya uvuguvugu,
1.  Hurahisisha umeng’enywaji wa chakula,
Maji ya moto ama vuguvugu katika kikombe uamkapo asubuhi inaweza kukusaidia mwili wako kuweza kutoa nje sumu katika mwili wako. Maji na vimiminika vingine husaidia kuvunja vunja chakula katika tumbo na kuweka mfumo wa chakula kuwa katika hali nzuri ndani ya mwili. Maji moto au vuguvugu husaidia kuweza kuvunja vunja chakula hicho kwa uharaka zaidi, na hivyo umeng’enywaji wa chakula kuwa mwepesi na kwa haraka.
Unywaji wa maji ya baridi wakati wa ama baada cha mlo wako inaweza kusababisha kusaidia kugandishwa kwa mafuta ambayo unayapata kupitia chakula na hivyo kusababisha mrundikano wa mafuta katika utumbo.
Uongezwaji wa barafu ili kutengeneza maji ya baridi hufanya kubadili mfumo halisi wa madini na virutubisho katika mwili, anasema Metsovas, ambavyo madini hayo ni muhimu ili kuweza kuuweka mfumo wa chakula katika hali ya afya, ambadani unaweza kufanya njia mbadala kwa kunywa chupa ya maji ya baridi sambamba na chupa ama glasi ya maji ya uvuguvu au moto ili kusaidia umeng’enywaji wa chakula, hususani baada ya kula mlo wako.
3. husaidia kulainisha choo
Kwa pointi moja au nyingine, wengi wetu tunakabiliwa na vidonda hususani matatizo ya tumbo ambapo huwa na choo kidogo au kukosa kabisa haja kubwa.
Vile vile ugumu wa haja uendapo choo wakati wa kukitoa, husababisha kuchanika kwa eneo la haja kubwa, haya yote yana letwa na ukosefu wa maji katika mwili. Unywaji wa maji moto au vuguvugu nyakati za asubuhi wakati tumbo likiwa halina kitu inaweza kusaidia utumbo mpana kuweza kusukuma uchafu/ kinyesi vyema na hivyo kusaidia kuwe na choo laini {kinyesi chepesi} wakati wa uvunjwaji wa chakula na hata usafirishwaji wake huwa mzuri kupita katika utumbo. Hivyo uchangamshwaji wa utumbo na maji moto husaidia kuurudisha mwili katika ufanyaji wake mzuri na wakawaida wa kazi vyema.
3. huodoa maumivu
Maji ya moto au vuguvugu, tukizingatia ni maji asilia ambayo wengi wetu katika majumba hutumia, husaidia kuondoa maumivu ya tumbo la hedhi kwa wakina mama na maumivu ya kichwa.

Umoto toka kwenye maji moto huweza kuwa na athari chanya katika misuli ya tumbo, ambayo huweza kusaidia kuondoa papo kwa papo makazo na misuli kujinyoosha. Kwa mujibu wa Healthline, wanasema maji moto au vuguvugu ni mazuri kwa maumivu, na kimiminika cha moto huongeza mzunguko wa damu kwenye ngozi na hivyo kusaidia kushusha maumivu ya misuli.
4. Husaidia kupunguza uzito
Kama uko katika mlo wako, unywaji wa maji nyakati za asubuhi basi inaweza kukusaidia katika kupunguza uzito. Maji moto ama uvuguvugu husaidia kuongeza joto la mwili, ambapo huongeza metabolic/ kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili. Kadiri kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili kinapoongezeka huruhusu mwili kuweza kuchoma kalori nyingi katika mwili. Hivyo husaidia figo na gastro intestinal kufanya kazi vyema katika mwili.

 “madaktari wana shauri kuwa unywaji wa maji moto nyakati za asubuhi, kila siku, pamoja na limao ndani yake, au chai huondoa vitu hatari katika mwili”.anasema Metsovas. Unywaji wa glasi kadhaa za maji ya moto au vuguvugu na limao ndani yake husaidia kuvunja vuja tisu za mafuta, katika mwili na hivyo husaidia mmeng’enyo wa chakula.
5. Huboresha mzunguko wa damu
Mrundikano wa mafuta katika mwili huondolewa wakati wa unywaji wa maji ya moto. Hii husaidia kuondoa sumu ambazo huwa zimezunguka katika miili yetu kwa kufanikisha mzunguko wa damu.
 Hakikisha misuli inapumzika na hivyo wakati kunapokuwa na mzunguko mbovu wa damu katika mwili wako.
6. Hupunguza hatari ya kuzeeka mapema

Hii inaweza kuzuilika kwa kunywa maji moto ama vuguvugu, upatikanaji wa sumu katika mwili hupelekea kuzeeka mapema na kwa haraka, lakini maji moto ama vuguvugu inaweza kusaidia kusafisha mwili kwa kutoa hizo sumu, hata hivyo pia kuirekebisha ngozi kwa kuoneza SelI mpya maeneo ya ngozi. Metsovas aliliambia jarida la Medical Daily  “wanawake siku zote hunufaika kwa sababu wanakuwa na homoni nyingi zaidi ambazo huhusika kwayo,”

          Kuweza kuwa ama kuongeza uimara wa afya yako kupitia unywaji wa maji moto ama vuguvugu, kunywa kila siku asubuhi maji pekee au yaliyochanganywa na limao kwa kuongeza radha. Metsovas anakubaliana na wanywaji wa maji vuguvugu au moto kwa, kadiri wanavyokunywa  maji moto wanaweza kuwa wana angamiza tisu za mdomo na hata maeneo ya kolomeo.  Baada ya kuuguzwa na maji hayo ya moto,
          Basi huna budi kuyaacha yapoe kidogo kabla ya kuanza kuyatumia kwa kuyanywa.

          Vile vile anashauri “ kila mara mwone daktari kwa maelezo kabla ya kuanza kunywa  maji hayo ya moto, kama utakuwa katika matumizi mengine ya dawa ambayo inaweza kuleta madhara katika ufanisi wa dawa hiyo” anasema metsovas.

Comments

Popular posts from this blog