Posts

BREAKING NEWS: WAJERUHIWA KATIKA VURUGU DUMILA.

Image
WATU kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea jioni hii huko Dumila mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo polisi wameingilia kati na kutumia mabaomu ya machozi kutuliza ghasia hizo.  Chanzo cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja aishiye Kijiji cha Mketeni wilayani Kiloasa wakati akibishana na mfugaji ambaye ni kabila la Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo.  Kufuatia kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata wenzake na kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi ya wafugaji wa eneo hilo.Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya wafugaji kukimbia, wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya Morogoro - Dodoma ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili huku wakichoma matairi Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima ambao pia walikuwa tayari wamevamia baadhi ya nyumba za kulala wageni zinazomili

DUNIA IMEKWISHA: BINTI AKUTWA AKIFANYA JARIBIO LA KUMLA MTOTO WAKE BAADA YA KUJIFUNGUA!

Image
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Li Zhenghua 24, amekutwa akifanya jaribio la kumla Mtoto wake aliyejifungua siku chache zilizopita, baada ya kumkuta taya yake ikiwa imenasa kuzunguka Mkono wa Mtoto wake.  Tukio hilo la ajabu lilitokea katika Hospitali iliyoko Shenzhen Kusini mwa jimbo la Guangdong, China ambapo mwanamke huyo alifikishwa kujifungua na baadaye wahudumu wa Hospitali kufanya jitihada za kutafuta ndugu zake.  Hata hivyo mwanamke huyo akiwa na siku ya tatu Hospitalini hapo alikutwa na nesi akiwa katika jaribio la kumng’ata mtoto ambapo madaktari walitumia nguvu na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye tayari alikuwa na jeraha mkononi.

MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAFANA JIJINI DAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange. Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mri

BILIONEA EMAMI WA NIGERIA AMPATIA TAYO DOLA 350,000/= KAMA BACKUP BAADA YA KUSHINDWA KWENYE SHINDANO LA BBAHOTSHOTS

Image
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255765957698 au email: pharsnyanda@gmail.com .  Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. Mshindi wa pili wa  BBAHotshots, Tayo Folarin   Baada ya East Africa yote kuinua shangwe kubwa siku ya Jumapili Desemba 7 kusherehekea ushindi wa nguvu alioupata Mtanzania   Idris   kwenye  BBAHotshots , kulikuwa na story kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazikuwapendeza watu wengi kwani ilionekana kama baadhi ya watu kama Nigeria hawakuwa na amani kuukosa ushindi huo na kuuona ukija Tanzania. Bilionea  Ayiri Emami Sasa mpya kutoka Nigeria ni kwamba bilionea mmoja hakupendezwa kumuona mwakilishi wao Tayo akiambulia patupu, bilionea huyo  Ayiri Emami  amempatia  Tayo Folarin  pesa ambazo ni zaidi hata ya kiwango ambacho kimetolewa na  BBAHotshots  kwa mshindi wa kwanza.  Tunawafahamu mabilionea wachache k

BREAKING NEWS: WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA HELIKOPTA HUKO GOMBO LA MBOTO JIJINI DAR!

Image
Muonekano wa Helikopta eneo la Gonga la Mboto jijini Dar.  Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya Helikopta kuanguka. Helikopta imeanguka leo eneo la Gongo la Mboto, Moshi Bar jijini Dar, kuna watu wanadaiwa kufariki dunia lakini polisi hawajatoa taarifa rasmi juu ya tukio hili.

HATIMAYE LADY JAY DEE AKIRI KUMUACHA MUMEWE GADNER HABASH - MSIKILIZE HAPA

Image
Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe kuwa ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G Habash imevunjika. Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner. Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner lakini alisema alikuwa akiteswa. Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa siku zote amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi kwenye vyombo vya habari.“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye media, kwenye magazeti au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote wanachohisi, chochote wanachotaka kusema.  SOMA ZAIDI>>>>

ANGALIA PICHA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA ARUSHA LEO

Image
Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru. Akiongea na mwandishi wetu mmoja ya mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani -Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na lori hilo. Habari kamili zitawajia punde. 

MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA SHERIA NGOWI AKUTANA NA RAIS JAKAYA KIKWETE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
 Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi (kulia) akibadilishana mawazo na Rais Jakaya Kikwete IKULU Leo Jijini Dar es Salaam alipomtembelea na kujadili mambo mbalimbali.  Rais Jakaya Kikwete akijadiliana na Ujumbe Maalum Ukiongozwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi (wa kwanza Kulia) ikulu jijini Dar es Salaam Leo   Rais Jakaya Kikwete akipitia baadhi ya sampuli za vitambaa vya nguo vinavyotumiwa na mbunifu wa mavazi wa kimatafaifa Sheria Ngowi (kulia)IKULU Jijini Dar es Salaam LEO,Kushoto ni Makamu wa Rais wa Sheria Ngowi Brand Haki Ngowi. Rais Jakata Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe Maalum Kutoka Sheria Ngowi Brand Ukiongozwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Sheria Ngowi (wa pili kushoto) Makamu wa Rais wa Sheria Ngowi Brand Haki Ngowi (wa pili Kulia) Mkuu wa Kitendo cha Biashara na Matangazo Deo Kessy (wa kwanza kushoto) na Kiongozi wa idara ya habari kutoka Sheria Ngowi Brand Atunza Nkrulu (wa kwanza Kulia). Picha na

ZITAMBUE 'NJIA KUMI ZA HARAKA KUONDOA “STRESS” NA UCHOVU'

Image
                                                              1 . Pitia picha zako zako  za zamani kidogo,  Picha za tukio moja wapo lililokufurahisha au za      mtu mwingine yeyote wa karibu yako                                                                 2 . Fungua madirisha na kuruhusu mwanga na hewa kupita kwa kiasi kikubwa. Epuka kukaa sehemu yenye mwanga mdogo kwani hufanya hali yako ya uchovu au stress kuwa juu zaidi.                                                                  3 . Imba huku unaoga! Sio lazima uwe muimbaji mahiri bali chagua tu wimbo wako unaoupenda, imba kwa namna yeyote huku ukiendelea kuoga                                                                   4. Epuka kubaki mpweke. Tafuta mtu yeyote uongee nae (hata mtoto mdogo) itakusaidia kupunguza mawazo au uchovu                                                                     5 . Sikiliza muziki au mpigie simu rafiki yako mliyepotezana muda mrefu.      

UKAWA WAMVAA RAIS KIKWETE TENA,WAIBUKA NA WASEMA MAZITO

Image
 Na Karoli Vinsent        SIKU moja kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kufikia Maazimio na Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA  kulisitisha bunge Maalum la katiba na kupisha Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo ya Mwaka 1977,             Nao Umoja huo wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA umeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo mara moja na kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4,kwani kufanya hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa za Wananchi,               Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la kujadili maazimio kati ya    viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),na Rais Jakaya kikwete uliomalizika Juzi

DIAMOND ATWAA TUZO NYINGINE YA COLLABO BORA YA MWAKA

Image
Tuzo waliyopata Dezert Eagle na Diamond Platnumz. Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'. STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametwaa tuzo nyingine ya Afro-Australia

MTOTO APIGWA KIKATILI NA BABA'AKE..AFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA!

Image
Mtoto Amani Elisha (10) aliyepigwa vibaya na baba yake mzazi hadi kuzimia kwa siku mbili.   KATIKA   hali ambayo siyo ya kawaida iliyowashangaza wakazi wa eneo la Ukonga Mazizini kwa Makobe, baba  mmoja aliyefahamika kwa jina la Elisha Zakari amedaiwa kumpiga mwanaye wa kumzaa kip i go kama cha ng’ombe machungani na kusababisha azimie na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto huyo aliyepigwa ni Amani Elisha (10) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Maarifa iliyoko Ukonga, Dar es Salaam, baada ya kipigo alizimia siku mbili.  Tukio hilo la kikatili lilitokea usiku wa Ijumaa iliyopita na sababu ya mtoto huyo kupewa kipigo inadaiwa ni kutokana na utoro shuleni na kwamba hata akienda huwa haandiki.Waandishi wetu waliponasa tukio walimtafuta mama mzazi wa mwanafunzi huyo maarufu kama mama Amani na mahojiano yakawa hivi:  Mwandishi: Mama ni kweli kuwa mume wako alimpiga mtoto wenu? Mama Amani: Ni kweli baba yake Amani ndiye aliyempiga. Mwandishi: Kwani

MOTO WATEKETEZA BWENI SHULE YA AFRICAN MUSLIM MJINI MOSHI HIVI SASA

Image
 Bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya African Muslim iliyopo Laloleni manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro linateketea kwa moto hivi sasa. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo umeanza majira ya saa 2 za usiku huku chanzo chake bado hakijajulikana na ripota wetu Dixon Busagaga aliye eneo la tukio anafuatilia ajali hii na atatujulisha kila kitachojiri na kupatikana. Kikosi cha zimamoto kimefanya jitihada za kuzima moto huo licha ya kukabiliwa na changamoto ya maji.

TAHADHARI...HUU NDIO UGONJWA UTOKANAO NA KUNYONYANA SEHEMU ZA SIRI

Image
MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO, NI CHANZO KIKUU CHA  SARATANI YA KOO? Saratani imeendelea kuwa tishio hapa nchini huku hofu ikiendelea kuikumba jamii kutokana na wataalamu wa afya kushindwa kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari. Takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha ongezeko la saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012. Mkurugenzi wa Idara ya Kinga  Ocean road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. “Saratani ya mdomo ipo, na nyingine zinasababishwa na zinaa “ anasema Dk Mwaiselage Tafiti za saratani Tafiti mbalimbali zimewahi kufanyika nchini na kubaini kuwepo kwa ongezeko la saratani ya mdomo.Utafiti uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini aina za saratani 1,594, kati ya hizo 509 zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003 pekee.

VYAMA VYA SIASA VINAVYOUNDA TCD VYATOA TAMKO KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA NA UCHAGUZI MKUU WA 2015.

Image
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma. VIONGOZI Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) wameku wa katika mashauriano ya zaidi ya mwezi mmoja tangu tarehe 2 Agosti mwaka huu huku wakishauriana juu ya mwenendo wa mchakato wa Katiba Mpya na jinsi ya kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki hapo mwakani Akiongea kwa niaba ya viongozi wengine wa kituo hicho, Mwenyekiti wa TCD, Mhe. John Cheyo amesema kuwa Katika mashauriano hayo yaliyochukua sura ya Kamati ya Makatibu Wakuu, Kamati ya Wenyeviti wa Vyama vya CCM, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi katika hatua tofauti. Mhe. Cheyo ameeleza kuwa kamati zote zilitoa taarifa zao kwenye vikao vya Viongozi Wakuu wa Vyama (Summit) ya TCD ambayo wajumbe wake ni Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama wanachama. Mhe. Cheyo aliongeza kuwa katika kutafuta maridhiano, Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama walifanya mashauriano na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete siku ya tarehe