MWIMBAJI MWINGINE WA KWETU PAZURI APATA MWENZA
Katika shangwe za GK siku ya leo, tunakupa picha chache kutoka Kigali nchini Rwanda, ambako mmoja kati ya waimbaji wa muda mrefu wa kundi la Ambassadors of Christ a.k.a Kwetu Pazuri aitwaye Furaha Sandrine , jumapili iliyopita aliutambulisha rasmi ubavu wake uitwao Ngabo Karangwa Tony katika sherehe ya kulipiwa mahari na kuvishwa pete ya uchumba rasmi iliyofanyika nyumbani kwao maeneo ya Gikondo jijini Kigali, ambapo harusi inatarajiwa kufanyika tarehe 6/7/2014 katika kanisa la Wasabato la Gisenyi na kufuatiwa na shere ya kuwapongeza itakayofanyika katika pwani ya Lac Kivu beach.
Comments
Post a Comment