MGIMWA ATUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUWATEMBELEA WANANCHI
Mbunge
wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa akitumia usafiri wa
Baiskeli kuwafikia wapiga kura wake katika kijiji cha Kivalali kata ya
Ifunda baada ya gari lake kupata pacha wakati wa zikara hiyo hivyo
kulazimika kutafuta baiskeli ili kufika haraka mkutanoni kusikiliza kero
za wananchi wake ,amini ni mbunge wa kwanza mkoa wa Iringa kutumia
usafiri kama huu kuwafikia wananchi wake,picha nyingine akisalimianana
wananchi wa kijiji Kivalali (picha na Francis Godwin Blog)
Na Francis Godwin, Iringa
MBUNGE
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa amevunja rekodi ya wabunge wa
jimbo hilo na majimbo mengine ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa kuachana
na matumizi ya magari ya kifahari na kuamua kutumia usafiri wa Baiskeli
kuwatembelea wapiga kura wake.
Huku wananchi wa kata ya Ifunda na Mgama wakisema kuwa ubunge wa
Mgimwa si wa mwaka mmoja ama mitano bali hadi mwaka 2025 hadi mwenyewe
atakavyo sema yatosha .
Mbunge Mgimwa atumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia wapiga kura ,wao wasema hawahitaji mbunge mwingine hadi 2025
Mbunge huyo alifikia hatua hiyo jana baada ya mmoja kati ya magari
yake mawilio yaliyokuwa katika msafara wake kukwama kulazimika kutumia
usafiri huo wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kuwatembelea wapiga
kura wake na kupokea changamoto mbali mbali
Alisema kuwa amelazuimika kuumia usafii huo ili kuwafikia wananchi
wake kwa wakati kutokana na gari lake kupata tatizo japo aliasema
usafiri huo ni wa kawaida kwani amekuwa akiutuimia toka utoto wake na
kuwa kazi ya ubunge si kujitenga na wananchi bali kuwa karibu nao kwa
mazingira ambayo wao wamekuwa wakiishi .
Mgimwa alisema kuwa katika ubunge wakle kamwe hatajitenga na
wananchi wake na badala yake ataendelea kuwa karibu nao kwa kuishi kama
wao wanavyo ishi ili kujua changamoto zao badala ya kutumia usafiri wa
magari kila wakati .
Alisema kuwa si kawaida kwqa mbunge kutumia usafiri huo wa Baiskeli
ila kwa kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi ni lazima kuwa tayari
kutumia usafiri wowote kulingana na mazingira na kuwa kamwe wana
Kalenga wasitegemee kuwa walikosea kumpa ubunge ila wanapaswa kuendelea
kujivunia kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwani ni nafasi ambayo anaipenda
na kamwe hatawaangusha katika kuwatumikia .
Japo aliwataka wana kalenga kuepumka kubadili wabunge kama nguo zao
kwani kufanya hivyo ni kujirudisha nyuma katika maendeleo na kuwataka
kujifunza kutoka katika majimbo ambayo wabnunge wake wameongoza kwa
zaidi ya vipindi vitatu na maendeleo yameonekana .
Pia alisema kuwa huu si wakati wa wana kalenga kuwakumbatia wale
ambao wanajipitisha kutaka kuungwa mkono mwaka 2015 na badala yake
wanapaswa kuwachukia watu hao na kuwaogopa kama ugonjwa wa ukoma kwani
fedha wanazotoa kwa sasa ni fedha ambazo wanawakopesha kwa riba kuibwa
ya kutaka ubunge ili kurudisha fedha hizo na sio kuwatumikia wananchi.
Mwisho
Comments
Post a Comment