YALIYOJIRI KWENYE MSIBA WA DIRECTOR WA FILAMU ADAM KUAMBIANA!

Mwili wa Adam Kuambiana ukiandaliwa tayari kwa kuagwa nyumbani kwake Bunju B jioni hii.



Waombolezaji wakiwa msibani tayari kuaga mwili. Wa tatu kutoka kulia waliokaa mbele ni mke wa marehemu Janeth Rithe ambaye ni Diwani Kata ya Kunduchi, Dar.

Watangazaji Sauda Mwilima (kulia) na Zamaradi Mketema (kati) wakiwa msibani hapo. Kushoto ni msanii Shamsa Ford.
William Mtitu (katikati) akiwa na waombolezaji.
Ibada ya kumuombea marehemu ikiendelea.
Mwili wa marehemu Adam Kuambiana ukitolewa kwa ajili ya kuagwa.
Baadhi ya wasanii baada ya kuwasili Bunju B.
Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani Bunju B.
Mwili wa marehemu ukishushwa kutoka kwenye gari Bunju B.
MWILI wa mwongozaji na mwigizaji wa filamu Bongo, Adam Kuambiana umeagwa nyumbani kwake Bunju B, Dar ambapo ndugu, jamaa, wanasiasa, marafiki wameshiriki tukio hilo. Kesho asubuhi mwili utapelekwa Viwanja vya Leaders kuagwa na baadaye kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar

Comments

Popular posts from this blog