MUUGUZI MWENYE HIV AFUNGWA JELA UGANDA
Muuguzi Namubiru aliambia mahakama hakuwa na nia ya kumuambukiza mtoto huyo HIV
Nchini
Uganda mahakama imempata na hatia muuguzi mwenye HIV, aliyeshitakiwa kwa
kumdunga mtoto mchanga sindano, ambayo awali ilimchoma yeye mwenyewe.
Muunguzi
huyo, Rosemary Namubiru, mwenye umri wa miaka 64, mwathiriwa wa virusi
vya HIV, amefungwa miaka mitatu jela, kwa kile hakimu amekiita, 'uzembe
wa weledi'.
Hukumu
hio imetolewa wiki moja baada ya bunge la Uganda kupitisha muswada,
unaomtia hatiani mtu yeyote ambaye kusudi anamuambukiza mtu mwengine
virusi vya ukimwi.
Mtoto huyo hata hivyo hakuambukizwa virusi vya HIV na wanaharakati wamekosoa mahakama kwa kumfunga jela mwanamke huyo.
Baba
huyo, Daniel Mushabe, amesema kuwa anatumai kesi hiyo itampa motisha
Rais Museveni kuidhinisha mswada uliopitishwa na wabunge wa kuwachukulia
hatua za kisheria watu wanaowaambukiza wengine HIV kusudi.
Adhabu ya kosa hilo ni faini ya dola 1,900 au miaka kumi jela.
Sheria hiyo ikiwa itapitishwa itawaadhibu wanaotenda uhalifu huo kwa maksudi.
Wananchi bila shaka walionyesha kuudhiwa na kitendo cha muuguzi huyo ingawa wanaharakati wamemtetea mama muuguzi.
Hakimu aliyetoa hukumu alisema kuwa Namubiru alikosa kuonekana kama aiyesikitishwa na kosa lake.
Namubiru, muuguzi mwenye uzoefu wa kazi wa miaka 30, alisisitiza kwamba hana hatia na kuwa mtoto huyo hakuambukizwa HIV.
Namubiru
aliamua kumdunga sindano mtoto huyo kutafuta mshipa lakini kapata ugumu
na hivyo kujidunga mwenye kwa bahati mbaya lakini amesisitiza kuwa
hakuwa na nia yoyote ya kumuambukiza mtoto huyo virusi vya HIV.
Rais anasubiriwa kuidhinisha au kutupilia mbali mswada wa adhabu kwa wanaombukiza wengine HIV kusudi
source:bbc
Comments
Post a Comment