HOMA YA DENGUE YABISHA HODI MBEYA, MGONJWA ALAZWA HOSPITALI YA MKOA
HATIMAYE
ugonjwa wa homa ya Dengue umeripotiwa kuingia Mkoani Mbeya baada ya
kupatikana kwa kesi ya mgonjwa mmoja mwanamke ambaye amelazwa katika
Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Mwanamke
huyo ambaye ni mkazi wa Sae, Jijini hapa, ambaye hata hivyo hakuwa
tayari jina lake liandikwe gazetini inasemekana alipata ugonjwa huo
baada ya kung’atwa na mbu aina ya Aides alipokuwa akiishi , Jijini Dar
es salaam.
Mganga
Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Gloria Mbwile, alithibitisha kupokelewa
kwa mgonjwa huyo na kwamba tayari hali yake imeimarika baada ya
madaktari kumpatia matibabu baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
Amesema mgonjwa huyo alifikishwa hospitalini hapo Mei 17 majira ya mchana, huku akionesha kuwa dalili zote za ugonjwa huo
Amesema
kutokana na hali hiyo madaktari walianza kuchukua hatua za haraka kwa
kuchukua sampuli za vipimo kwa ajili ya kuvipeleka Dar es salaam kwa
uchunguzi zaidi, wakati huo huo wakimtoa katika wodi ya wagonjwa
mchanganyiko na kumpeleka ile ya binafsi.
Dk.
Mbwile amesema hali ya mgonjwa huyo imeimarika baada ya kupatiwa
matibabu ya kina na kwamba hiyo jana angeweza kuruhusiwa kutokana
hospitalini hapo.
Hata
hivyo, Katibu wa afya Mkoa wa Mbeya, Juliana Mawalla, amewataka
wananchi wa mkoa wa Mbeya kutoa hofu juu ya ugonjwa huo kwani mgonjwa
huyo alipata maambukizi hayo akiwa Jijini Dar es salaam na kwamba tayari
serikali imeleta vifaa kwa ajili ya vipimo katika hospitali ya mkoa na
ile ya kanda ya Rufaa Mbeya.
Kwa
upande wake Mama mzazi wa mgonjwa huyo, ambaye naye aliomba jina lake
lihifadhiwe, amesema mwanae alifika Jijini Dar es salaam Mei mosi mwaka
huu kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya dada yake na alikaa huko kwa siku
nane.
Dengue
ambayo tayari imeshaua watu watano mpaka sasa , huku wagonjwa zaidi ya
400 wakiwa wamegundulika kuambukizwa na kupatiwa matibabu ya ugonjwa huu
katika mkoa wa Dar es salaam hali ambayo imeibua hofu kubwa kwa
wananchi.
Comments
Post a Comment