Angalia Picha Kijana Afia kaburini wakati akijaribu kufukua maiti

Maiti ya kijana huyo ikiwa imenasa kaburini

ukio la ajabu na la kushangaza limetokea huko nchini Nigeria baada ya kijana mmoja kukutwa akiwa amekufa kaburini,kijana huyo alikumbwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina.

Kwa mujibu wa mtandao wa Saturday Tribune wa Nigeria, tukio hilo limetokea katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi walikimbia na kumuacha akihangaika kujinasua,lakini jitihada zake ziligonga mwamba mpaka pale umauti ulipo mkuta.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi huku kichwa chake kikiwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hilo waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.




Mtandao wa Saturday Tribune ulibaatika kuongea na kamishina wa Jeshi la Polisi wa eneo la Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilipelekea kijana huyo kupoteza maisha.



Msemaji wa jeshi hilo aliongeza kuwa mpaka sasa jeshi lake bado halijathibisha kwamba tukio hilo limetokana na masuala ya kishirikina.

Comments

Popular posts from this blog